Kampuni
inayoongoza kwa burudani barani Afrika, M-Net inazindua chaneli mpya yenye kulenga watanzania, itakayokuwa na burudani
mbali mbali zenye hadhi ya Kitanzania,
ni MAISHA MAGIC BONGO itakayoanza
kuonekana hewani Octoba 1 saa 10 Alasiri. Moja ya madhumuni ya M-Net ni kuhakikisha
inalifikia soko la wateja wake ikiwemo kuingiza maudhui wanayopenda wateja wake.
Chaneli hii mpya inategemea kukidhi mahitaji ya soko la wateja wa Tanzania.
Ikihusisha
vipindi zaidi ya 6 vitakavyokuwa vikiruka kila siku, MAISHA MAGIC BONGO itakuwa
inapatikana kwa wateja wote wa Afrika Mashariki
kupitia chaneli 160. Mbali na
kuonyesha filamu kali kutoka Bongo Muvi na tamthilia za Kiswahili zinazopendwa
na kufatiliwa nchi nzima, chaneli hii pia itakuwa ikionyesha vipindi vya maisha
ya wa Tanzania, Muziki ukiwemo Bongo
Flava , Maisha ya Mastaa na vipindi vya majadiliano ya moja kwa moja , bila
kusahau sinema kali za kihindi kutoka Bollywood zilizotafsiriwa kwa lugha ya
Kiswahili.
Akizungumza juu
ya uzinduzi wa 'MAISHA MAGIC BONGO, Mkurugenzi wa M-Net kwa Afrika Mashariki
Theo Erasmus anasema, " Tumefurahi kufunua mkondo huu mpya na kwa
kuendelea mbele tunatarajia chaneli hii itakuwa moja ya chaneli pendwa zaidi
Tanzania kwa msaada wa watazamaji wetu wa Tanzania ambao daima wamekuwa
waaminifu kwetu na ndio sababu M-Net leo tumeamua kuwaletea chaneli hii mahususi
kwa ajili yao.
Tunashukuru
zaidi tumeweza.
kupata baadhi ya
vipindi bora kutoka kwa wazalishaji wakubwa kutoka ndani ambao wanashirikiana
nasi, pia tunaangalia namna ya kupanua ushirikiano wetu zaidi na wazalishaji
hawa wa filamu na vipindi vya runinga ili kuhakikisha kwamba mafanikio yao
yanakuwa makubwa zaidi.
Ni mwezi sasa, tangu
DStv ilipotangaza kwenye maonyesho ya maudhui nchini Mauritius, MAISHA MAGIC
BONGO ipo tayari kuzinduliwa, na baadhi ya vipindi vitakavyokuwemo kwenye
chaneli hii ni:
- Filamu za kibongo zitaonyeshwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa
saa 17:00 jioni, pia Jumamosi na Jumapili saa 19:30 usiku. Wakati huo huo Filamu za kihindi
zilizotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili zitakuwa zinaonyeshwa kila siku ya
Ijumaa saa 19:30 usiku. Baadhi ya Bongo Muvi maarufu zilizopo kwenye
ratiba sasa ni Hard Price, Jimmy,
Nampenda Motika na Nusra, na baadhi ya za kihindi ni I am 24, Jimmy, Anwar na Amar Akbar Anthony.
Upande wa Tamthilia , jiandae kupata Talaka ( Jumanne saa 19:00 usiku ), usikose Mtaro ( Jumatatu saa 19:00
usiku) Isiyopitwa na muda Siri ya Mtungi ( Jumamosi na
Jumapili saa 18:00) na ya vijana
zaidi Dunia Tambara Bovu ( Ijumaa saa 19:00 usiku). Wasanii wenye
vipaji waliopo kwenye tamthilia
hizi ni kama vile Hamis Korongo , Alafa Arobain , Paulo Francis, Juma
Rajab Rashid, Hidaya Maeda, Daudi Michael, Caroline Hussein na Habibu
Seif na wengine wengi, hakika hii
si ya kukosa!
- Bila shaka, MAISHA MAGIC BONGO pia itakuletea vipindi viwili vya muziki, Mzooka (Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 Alasiri) itakupa burudani ya video mpya kali kutoka Bongo, wakati kipindi cha Sifa Mix kitakuwa kikikujia ( kila Jumapili saa 11:00 asubuhi) ikikuletea muziki laini wa nyimbo za Dini.
- Pia kuna vipindi majadiliano utaviona kwenye chaneli hii, kama vile Mkasi ( kila Jumapili saa 16:00 EAT ) ambazo inazungumzia maisha ya wasanii wakubwa Tanzania, kisha hakikisha hauachi kumfuatilia Mboni (Jumamosi saa 15:00 EAT) Mboni Masimba akifanya mahojiano na watu mashuhuri , wajasiriamali, viongozi wa jamii na siasa , kujadili mada mbalimbali kuanzia utamaduni wa kiuchumi.
- Pia kwenye MAISHA MAGIC BONGO, usikose kuangalia kipindi cha Ajabu, kinachoburudisha na wakati mwingine kuogopesha lakini muda wote kitakuburudisha (Jumatano saa 19:00 Usiku).
- Kwa kusherehekea uzinduzi wa Maisha Magic Bongo, DStv inafurahi kuwatangazia punguzo la bei kwenye vifaa vyake kuanzia tarehe 1 Oktoba 2015. Vifaa vya DStv sasa vitapatikana kwa Tshs 79,000 tu, vigezo na masharti kuzingatiwa.
Hii ni
kuwawezesha waTanzania kuangalia chaneli mpya ya Maisha Magic Bongo
itakayopatikana kwenye vifurushi vyote, ikiwemo kifurushi cha Bomba ambacho ni
Tshs 23,500 tu kwa mwezi.
Hivi pamoja na
vingine kibao ambavyo si vya kukosa kwenye
chaneli hii mpya, hakikisha
unaangalia MAISHA MAGIC BONGO kuanzia usiku wa leo! Tembelea tovuti www.maishamagic.tv kwa maelezo zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...