Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva  akizungumza katika mkutano na  vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mkurugenzi wa uchaguzi, Kailima Ramadhan akizungumza na wadau wa vyama vya siasa leo jiji ni Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia maada leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa  ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amevitaka vyama vya siasa kupeleka malalamiko yao katika kamati ya maadili ya NEC  na sio kwenda kutoa malalamiko yao  katika vyombo vya habari.

Lubuva aliyasema hayo leo wakati NEC ilipokutana na vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,amesema kuwa  nafasi vya siasa vina nafasi ya kuhamasisha watu wapige kura kwa wale wenye sifa.

Amesema wakati wa kupiga kura watu wakipiga kura wanatakiwa kuondoka na kazi zingine zitafanywa na mawakala ndio watakaofanya kazi zoezi la kuhesabu na baadae kubandika.

Lubuva amesema watu wakikaa vituoni wanaweza kuvuruga amani  na kufanya zoezi  la upigaji kura kuharibika.
Amesema tume imejipanga katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika  kwa uhuru na haki kutokana na mfumo  wa kisasa.
 
Aidha amevitaka vyama vya siasa kunadi sera zao  na sio kushughulika na watu kwani wananchi  wanahitaji sera waweze kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi.

Baadhi ya vyama vya siasa vimeridhishwa na ushirikishwaji wa NEC katika masuala kuelekea uchaguzi mkuu na jinsi walivyojipanga uendeshashaji wa uchaguzi mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...