Kundi la Mawakala wa utalii kutoka nchi mbalimbali limewasili jana jijini Dar es Salaam likitokea visiwa vya Zanzibar kwa ajili ya kushiriki onesho la kimataifa la Utalii lijulikanalo kama “Swahili International Tourism Expo”.
Onesho hili litafanyika kuanzia leo Oktoba 1 – 3, 2015 Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Mawakala hawa wanaojihusisha na kutoa huduma mbalimbali za utalii katika nchi zao, wamepata mualiko huu wa kuhudhuria onyesho la S!TE ili kuwapa nafasi ya kuvijuwa vivutio vya utalii vya Tanzania waweze kuwahamashisha watalii katika nchi hizo kuja kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.
Aidha, onyesho ili linatoa fursa kwa Mawakala wa Utalii wa Tanzania kuweza kufanya biashara na mawakala hao kutoka katika nchi mbalimbali duniani; Canada, Marekani, Ujerumani, India Ireland, Israel, China, Ethiopia,Uingereza, Australia na Afrika ya kusini.
Wadau wa utalii wa kimataifa wamepata fursa ya kuvitembelea vivutio vya utalii vya viziwa vya Zanzibar na baada ya maonesho watatembelea Hifadhi za Taifa za Tarangire, Manyara na Bonde la Hifadhi la Ngorongoro.
Onesho la S!TE limetayarishwa na Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Pure Grit ya Afrika ya Kusini. Onesho la kwanza lilifanyika tarehe 1-4, October, 2014, Mlimani City, Dar es Salaam.
Mawakala
wakiwasili katika bandari ya Dar es Salaam wakitoka visiwa vya Zanzibar.
Mawakala wakipata historia ya sehemu ilipokuwa ikifanyika biashara ya Utumwa Zanzibar.
1Mawakala wa utalii wakiingia katika kanisa la kihistoria “The Anglican Cathedral's Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...