Dr. Servacius Likwelile
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali wa kwanza kushoto akiwa
katika picha ya pamoja na Magavana wa Mashariki
na Kusini mwa Afrika baada ya mkutano wa
MEFMI
(Picha
na Eva Valerian, Peru – Lima).
KATIKA kipindi hiki
cha mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa,
kumekuwa na mikutano mbalimbali inaendelea hapa nchini Peru. Mikutano hiyo inaendeshwa
na Taasisi mbalimbali zenye utaalamu wa kiuchumi na kifedha. Akizungumza na waandishi
wa habari, katibu Mkuu Wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile alisema “MEFMI ni
chombo kikubwa kwa Afrika Mashariki na Kusini katika kutoa mafunzo ya usimamizi
wa mambo ya uchumi kwa watendaji wa nchi wanachama.”
Aliendelea kusema kuwa
katika siku hizi mbili wamekutana na chombo hicho kwa madhumuni ya kuzungumzia
maendeleo ambayo yanatokana na rasilimali kama vile gesi na madinii na
kutoa mapendekezo ya namna gani Afrika inaweza
kusimamia rasilimali hizo.
Akitoa ufafanuzi
katika majadiliano hayo Dr. Likwelile alisema”Tanzania kuna rasilimali nyingi kama
vile gesi ambayo imegunduliwa Mtwara na kusisitiza kuwa kuna nchi
mbalimbali barani Afrika ambazo zina dhahabu
ya kutosha ambayo inaweza kuinua uchumi wa Afrika kama kutakuwa na utaratibu
mzuri wa kuzitumia.
“Lengo kuu la
mkutano wa MEMFI ni kuzungumzia shughuli zinazofanywa na MEMFI ili kuwezesha kupanga
namna ya kuboresha uwezo na kuendesha shughuli zetu katika kuinua uchumi wa
Afrika kwani tutahitaji fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye miundombinu
lakini lazima tuhakikishe kwamba tunafanya hivyo ili kuhakikisha uchumi wetu
unakuwa imara na kunakuwa na utaratibu
wa kuweka akiba kwa ajili ya vizazi vijavyo, hili ni suala la msingi sana”
alisistiza Likwelile.
Likwelile aliongeza
kuwa “Vizazi vingi vinatumia rasilimali zote bila kuangalia utaratibu wawakati
ujao kuwa utakuwaje, hivyo katika kikao hiki tumekubaliana kuanzisha mfuko ambo
ni kwa ajili ya kuwekeza kwa ajili ya matumizi ya baadae (Sovereign Wealth
Fund). Masharti ya mfuko huoyatakuwa ni kama ifuatavyo: (i) Mfuko huo lazima
uweze kuzalisha ajira, (ii)Mfuko huo lazima uwe na misingi imara ya kusimamia
uendeshaji wa shughuli zake,(iii) Mfuko lazima uwe na chombo imara kinacho kisimamia
mfuko huo. (iv) Lazima kuwe na utaratibu ambao unasema mfuko huu utafanya nini
na hautafanya nini.
La msingi kuwe na
mfumo wa kisheria lakini tuangalie rasilimali watu ili kuweza kuhifadhi mfuko
huo. Na namna gani miundombinu itawezakusaidia kuimarisha uchumi ili uweze
kutambuliwa.”
Naye Gavana wa
Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu alisema kuwa,ni muhimu kujua mapato
yetu yatokanayo na upatikanaji wa madini kwani tunaweza kuyatumia vizuri katika
kuhakikisha tunatengeneza miundombinu, kuongeza uwezo wa kuzalisha na baada ya
hapo nchi iweze kuendelea kupiga hatua hata kama madini yatakuwa yamekwisha.
Waziri wa Fedha ni Gavana
katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji
Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande
wa Benki ya Dunia (WB), aidha Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni
Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Hali ya hewa mjini hapa ni baridi,
rasharasha na manyunyu ya hapa na pale hasa nyakati za asubuhi.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
Lima - Peru
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...