Tumewaita hapa kuwaomba muwaeleze Watanzania wenzetu, jumuiya ya kimataifa na marafiki zetu wengine wa ndani na nje, kwamba hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kote nchini.
Hii ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya wananchi.
Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli.
Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa.
Kwa mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na Mtambile, kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma, Same Mashariki, Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, siyo kura za uchaguzi mkuu wa rais. Tunaweza kuiita, “mzimu wa uchaguzi.”
Ndugu waandishi wa habari;
Tangu kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) – mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya rais,
Hata hivyo, Tume imeendelea kutangaza matokeo hayo, bila kujali kile ambacho tumekieleza na kukilalamikia, kana kwamba tunachokisema ni ujinga, uzushi na uwendawazimu. Hili halikubaliki.
Aidha, katika maeneo mengine, likiwamo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyoko mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi, yanatofautiana na yale ambayo yamekusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo.
Hali kama hiyo ipo pia katika majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA na wale wa vyama washirika vya CUF na NCCR – Mageuzi, ama wamekuwa na nguvu kubwa au wameibuka washindi.
Upo ushahidi wa wazi ambao, ninyi waandishi mnaweza kwa kutumia uandishi wenu kuuthibitisha kwamba, katika majimbo yote ambako wagombea wa UKAWA wameshinda, TUME imechelea kutangaza matokeo ya urais kwa sababu zinazothibitisha kuwapo kwa mikakati ya hila.
Ikumbukwe kwamba matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada tu ya Jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabia kura na kuwakamata wataalam wetu waliokuwa wakipokea matokeo ya kura za rais nchi nzima ambayo hadi uvamizi huo ulipofanyika tulikuwa tukiongoza katika maeneo mbalimbali.
Ndugu waandishi wa habari;
Tunaamini kwa dhati kwamba, uvamizi huo ulifanyika mahususi kwa malengo ya kufanikisha uchakachuaji huo ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa sasa na NEC.
Wakati tukijua kwamba NEC ndiyo mamlaka pekee ya kisheria ya kutangaza matokeo ya urais, tunapenda kuwataarifu Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati uvamizi huo ulipofanyika kura zetu za urais tulizokuwa tumezikusanya zilikuwa zikionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60.
Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na watendaji wa NEC, mimi Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, tunautangazia umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC.
Ndugu waandishi wa habari;
Kutokana na makosa hayo makubwa, tunaitaka NEC kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo ya urais na kuanza upya kufanya uhakiki wa kile wanacholetewa na wasimamizi wa majimbo ambacho ushahidi unaonyesha kuwapo kwa vitendo vya hila ambavyo vinafanywa na NEC.
Ndugu wana habari
Kile kinachofanywa na NEC hapa ndiyo kile kile kinachoendelea kufanywa kule Zanzibar leo na ZEC ambako kunafanyika juhudi kubwa na za makusudi kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa wazi wa ushindi wa Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF anayeungwa mkono na UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad.
EDWARD LOWASSA
MGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Nchi hii ni ya utawala wa kisheria kama hamkubaliani msilete tafrani, wala kuingilia kazi ya tume nendeni mahakamani.
ReplyDeleteAsiyekubali kushindwa siyo mshindani, tufuate taratibu zilizopo zakutafuta haki, tusije kuchoma nchi kama wenzetu miaka iliyopita, halafu tukajuta kama wao uchaguzi uliopita walipata hekima ya kutumia mahakama badala ya kuhamasisha wananchi kuvuruga amani kisa matokeo ya uchaguzi. Tumuunge mkono kiongozi ajaye nchi yetu iende mbele.
ReplyDeletekama Goodluck alivyofanya Nigeria tafadhali viongozi wetu muwe mfano kwetu mpigie mshindi atakayetangazwa ukimpongeza ili taifa liponye majeraha ya uchaguzi tuungane pamoja tulete mabadiliko kwa wananchi wote waliounga mkono vyama vyote nane.
ReplyDeleteHa ha ha! Mhe Mbowe anacheka! Anajua wamemrubuni na kumtumia Mhe Lowassa! Wamejiongezea viti vyao ambalo lilikuwa lengo lao. Mzee wa watu wanalia naye machozi ya mamba akioma mzoga! Pole Mzee kachunge ngombe tu sasa.
ReplyDeleteNyie hamna kitu kichwani,, hamjasoma na hata picha hamuoni"" ccm itazulumu xana haki zetu watanzania but ipo siku tutaonyesha hisia na maumivu yetu
DeleteTaifa la MUNGU halikiwa na aman ije iwe Tanzania,, amani gani unayoitaka ambayo huna ww"" kuna amani gani tz,,,,, fikiria kwa kina ndugu usiropokeropoke tu
I hate people kama ww xana
Jamani kuna watu wana uroho wa madaraka. Wewe umeshakatwa mara tatu ndani ya chama chako cha Mapinduzi. Umeenda nje na kununua chama, wananchi wamekukataa. Unataka mpaka uambiwe nini kuwa sio lazima uwe Raisi wa Tanzania? Je, kama madaia yako eti umeshinda umepata kura ngapi? Je umepata wabunge wangapi? Angalia hilo na jiangalie kwenye kikoo jibu unalo. Msitake kutuvurugia Amani ya nchi yetu kwa ulafi wenu wa madaraka. Mshindwe katika jina la Yesu Kristo. Amen.
ReplyDeleteMpenda Amani.
Tatizo no moja hapa tamaa ya madaraka na kutokuwa na vision ningependa kabisa kutotumia neno hili hila ninabidi niseme unaponzisha chama cha siasa in lazima use na vision na unapotaka kiungia kwenye siasa no lazima ujuwe misingi ya siasa na siyo kufikiria kwamba wewe unaakili kushinda watu wrote Mr Mbowe na chadema mlitegeneza chama cha ukabira chama cha ukasikazini ukifiri kwamba watanzania wengine hatuoni Leo hii na ukweli in were mbowe kwa kujifanya kuwa we we na lowasa na sumaye na mbatia in lazima mtawale lakini ukweli no kwamba maghufuri ameshinda clean sababu yuko na clean CV sio na lowasa ambaye CV take iko na madoa mengi Leo mnasoma umesahau damu in zito kuliko maji ccm awajasema kula za Arusha Moshi Kilimanjaro alizopata lowasa hazikuwa za haki in kula za haki sababu lowasa na nyinyi wrote in watu wa kaskazini he unafikiriaje kwa watu was kanda ya ziwa wako na haki ya kumpa mtoto wao kula zote hill mmesahau na mmesahau ccm hawtegemehe kula za mjini wanategemea kula za vijijini kati ya maghufuri na lowasa nani alitembea sana kwa barabara haya Luna kula za kinamama pia na hizo mmesahau no lazima mjue ccm walihesabu vizuri nyinyi mkakurupuka sababu ya lowasa kutaka kumuonyesha kikwete tunaomba msijaribu kutuharibia Amani Wala kutuvurugia nchi yetu Luna koti kama amkubari mwende kotini nasiyo kudanganya vijana heti mtuwapatia Kazi lowasa alishindwa hats kujibu maswali alipohojiwa na Bbc Mr Lowasa and Mr mbowe and Mr Mbatia don't you deserves what you have got because like late Mtikila use to say Apedomia you and your friends your sick .
ReplyDeleteI want to say to ukawa Tanzania Peoples are not stupid you have lost to Tonga Tinga .
Another weakness is We shall take you to ICC or UN or EU for your information this people they don't care about you what they care is money how are they going to make money from you.
Did EU help peoples of Rwanda 1994 no did UN help them no so stop thinking of kissing European ass .
Mr lowasa It is time you step out of this Game you have lost you can note even debate it time you go with peace don't spoil our country don't spoil our peace if you guys you cross the Red line the government should not hestate to use full force.
Bye bye Ukawa bye lowasa
Yusef
msituletee majonzi mnaleta enzi za mwaka 47 nyuma mfano timu za mpira za zamani wakishindwa basi anatokea mmoja anaweka mpira kwapani na kukimbia nao na mchezo ndio mwisho kubali matokeo wananchi wanaojielewa wamefanya maamuzi ya kweli. tulieni na mjipange upya kama mtaufikia uchaguzi ujao. kuweni wazalendo tumuunge mkono kiongozi wetu kwa kujenga nchi yetu ili isonge mbele, tushilikiane pamoja na tukosoane kwa mapungufu ili tujenge nchi yetu. hayo mnayo yafanya kwa mantiki ya nafsi zenu kuhamasisha vijana wafanye vulugu sio vizuri na ata Mungu hapendi tunakaa kwa wasiwasi kwa sababu ya midomo yenu maneno mnayohamasisha vijana wasiojielewa ili kuleta uvunjifu wa amani hatupendi na tumechoka na kauli zenu,atufanyi kazi zetu kwa amani kwa kuofia chochote cha weza tokea kufuatia kauli zenu za kuamasisha vurugu.angalizo iwapo kutatokea uvunjifu wa amani mkae mkijua hiyo dhambi itawavaa milele na milele mpaka kufa kwenu,asiye kubali kushindwa na siyo mshindani. makusudio yenu yalijionyesha toka mchakato kuanza mlianza kunadi kuibiwa kura na ata kabla kura hazijapigwa hivyo mlilijua ilo kuwa mtashindwa. tunahitaji amani ya nchi yetu nafsi zenu kaeni nazo tuachie nchi yetu kwa amani tuliyotunukiwa na Mungu - Amen
ReplyDeletehahahahahahaahahahahaaaaaaaaa! kazi ipo
ReplyDeleteAkili ni nywele kila mtu ana zake. AMANI KWANZA MENGINE BAADAEEE
ReplyDeleteHawajawahi kuona jeshi la wananchi wanavyotembeza mkong'oto, ngoja wajaribu waone cha moto. tuacheni na Tanzania yetu bwana, kubalini kushindwa. nyie waulizeni watu wa Burundi juzi juzi tu, achene kabisa kuja kututesea watoto wetu, wakati nyie mtakuwa majumbani mwenu na wake zenu, watoto wetu ndo kuwafanya makanyaboya.
ReplyDeleteAMANI AMANI AMANI TUNAHITAJI AMANI TANZANIA.
OLE WAKE AANZISHAYE VURUGU, CHA MOTO ATAKIONA.
Haki ifwate waone kama hao watasema kitu.acheni ushabiki,,watu wanaongeya logic..kama kule zimefutwa inamaana wameona zinamakosa sasa huku watatangaza vipi..wakishindwa wao ndio zirudiwe,,wngekuwa wameshinda am sure wangetangaza kule..jonathan alitenda haki ndio maana alikubali..
ReplyDeletehatujawahi kusikia hata siku moja chadema au cuf wakakubali kushindwa
ReplyDeleteUKAWA msiingilie kazi za tume nendeni mahakamani
WASANII NA WANANCHI TULISHA SEMA AMANI KWANZA,SASA WANASIASA MSITAKE KULITIA TAIFA KATIKA MGAWANYIKO KWA TAMAA ZA MADARAKA - AMANI KWANZA ,MSITUWEKE WANANCHI REHANI KWA UCHU WA MADARAKA,TUME IPO HURU LAZIMA IAMINIWE
ReplyDeleteCCM mbele kwa mbele!!!! Watanzania tumeamua! Msitucheleweshe tunataka kupaaaa na maendeleo sie Mzee Kingunge na Sumaye wapo wapi??
ReplyDeleteYeye alipaa na elikopta alizani kura zipo juu
ReplyDeleteNyie wote mnaondika hapa ni vibaraka wa chama kile cha majambazi, ni aibu. Siku moja watu wa hao hao mliowaibia huo uongozi watakuwa ahwana jinsi bali kufanya mapinduzi ya kweli kama ya sehemu nyingi tuzionazo duniani. Jipongezeni sana, lakini "za mwizi ni arobaini" Hamuoni mko peekeni yenu kutoa maoni?!!au labda ni mtu mmoja mmoja anarudia yale yale, unajitekenya mwenyewe. Kiingerzea chenyewe ukijui kama uanchafua hewa tu. Na wewe Michuzi usibanie hii maana hiyo nchi si ya kwenu pekee yenu.
ReplyDeleteNdugu msemaji wa mwisho, unawaitaje watu vibaraka, mi nadhani we ndio hujui elimu ya siasa. Wote tunapenda bunge la upinzani ili viongozi walio madarakani wasijisahau. Lakini kama ulitegemea lowasa angepita, ningeshangaa. Nikupe mfano mmoja, lowassa alipotoka ccm hakujiunga na chama chochote, na leo kasema kawatoa mawakala wake kwenye chumba cha kutolea matokeo ya urais, kamtoa wakala wa chama gani. I just read somewhere that vyama vilivyoshiriki uchaguzi zimesaini form ya kukubali matokeo kasoro chauma na chadema. Sasa yeye anawakilishwa na chama gani kama sio ubabaishi. Wote tungependa tz ipate maendeleo. Ila pia tunajua lowassa na kundi lake la majambazi ni la uroho tu wa madaraka
ReplyDeletendio maana tumemnyima kura na kula pia, hizo alizozikwapua zinatosha, na hao marafiki zake waliomchangia imekula kwao.
Acha jazba we mdau, hii ni nchi yetu lazima tuisimamie tunapoona wanasiasa wanataka kutupotosha hatuwezi kunyamaza.
ReplyDeleteHaya siyo mambo ya chama ni ya nchi yetu na watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama.
Kama mechi ya mpira wa miguu, kipenga kimelia, mshindi ametangazwa ni mtanzania mwenzako, na mpira umekwishaaaaa..hakuna dakika zanyongeza hapa kwa wakati huu. Iliyobaki ndugu yangu upinzani nao una wajibu mkubwa katika nchi hii ufanye kazi yake. Sisi watanzania wenzako tunakupenda uchaguzi umeisha ndugu yetu shirikiana nasi tujenge Tanzania moja. Ondoa hasira haisaidii..
hahaaaaaa mzee lowasa ,waambie kingunge na sumaye waka kusaidie ku chunga ng,ombe monduli
ReplyDeleteNdg WATANZANIA wenzangu wapenda amani tusikashifu wala kuwatukana viongozi wetu haki itatolewa na jumuiya ya kimataifa kama ni ccm ama ukawa tupende amani nchi ni yetu na MUNGU wetu hataiacha nchi hii iingie kwenye machafuko tunazikataa na kuzifunga hizo na kuzisweka kuzimu kwa nguvu na uwezo wa MUNGU wetu Amin
ReplyDelete