Mkurugenzi wa taasisi ya Mkubwa na Wanawe, Said Fella 'Mkubwa Fella' akiwa na baadhi ya mtoto katika hospitali hiyo.

Mkurugenzi wa taasisi ya Mkubwa na Wanawe, Said Fella 'Mkubwa Fella' akikabidhi msaada katika hospitali ya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam ikipokelewa na Dk. Silas Adam.

Mwandishi Wetu

TAASISI ya Mkubwa na Wanawe inayomilikiwa na Mkurugenzi wake Said Fella 'Mkubwa Fella' jana ilitembelea Wodi ya Wanawake na Watoto katika Hospital ya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na waandishi wa habari Hospitalini hapo ambapo alikuja kutoa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa sambamba nakufanya usafi katika eneo la hospitali hiyo.

Fella alisema, ameguswa kuitembelea hospitali hiyo na ataendelea kufanya hivyo kupitia umoja wa vikundi vya Joging saba alivyoviunda katika kata yake ya Kilungule anakowania Udiwani.

"Tumekuja hapa Hospitali kuwasalimia wagonjwa na tumewaletea kitu kidogo tulichojaaliwa kama unavyoona Sabuni, dawa za meno, soda, juice na vitu mbalimbali,"alisema Fella.

Akizungumzia msaada huo Dk. Silas Adam alimshukuru Fella kwa sapoti yake na kuona umuhimu wa kuwatembelea wanawake na watoto katika Hospitali hiyo.

Silas alisema, licha ya shukurani hiyo ya vifaa hivyo amemuomba Fella kuwasaidia damu kupitia vijana wake hao kwani wanachangamoto kubwa ya damu hasa katika wodi ya wazazi.

"Tunamshukuru sana Fella kwa kidogo alichojaliwa kukileta kwetu ni faraja kubwa sana kwetu, tunatambua alivyotoa mchango mkubwa kwa vijana hapa nchini. hivyo basi kupitia vijana wake hao tunakuomba utusaidie waje watoe damu,"alisema.

Aliongeza kwa kuwataka Watanzania wengine kuwa na moyo kama wa Fella kusaidia watu mbalimbali hata kama sio katika hospitali hiyo.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa vikundi hivyo vya jogging  Salimu Omary alisema wametembelea hospitali hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya kuzindua umoja wao kupitia kata ya Kilungule ambapo uzinduzi huo unafayika leo.



mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hiyo hospitali ni ya kishenzi imejaa rushwa Na huduma zao ni mbovu mwezi sasa hospitali haina dawa ukienda unapewa panadol haijalishi unaumwa nini pili gharana zao ni kubwa kama hospital bibafsi
    Pia ukihudumiwa hawatoi risiti naukipewa risiti bei ina andikwa tofauti naile uliolipa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...