Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (kulia) akipewa maelezo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu, Godwin Ogweyo kuhusu utengenezaji wa kadi ambazo hazichafui mazingira alipotembelea maonesho ya shughuli zinazofanywa na wanafunzi hao alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 46 ya wanafuzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kulia kwake ni Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.
Wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman wakati akiwasili ukumbini kuhudhuria sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi hao, shuleni hapo juzi (Oktoba 22).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Mhandisi Suleiman S. Suleiman akivishwa skafu na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu kama heshima ya kuwa mgeni rasmi katika sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.
Bwalo naona lina muda kidogo halijaona rangi. Mgeni rasmi aungane na wadau wengine wa Pugu tuone jinsi ya kuing'arisha kidogo shule yetu.
ReplyDelete