Msanii wa mziki wa Hip hop wa nchini Kenya ambaye pia ni Daktari nchini humo, Francis Hamis ( a.k.a Frasha) akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA Tower na waandishi wa habari kuhusiana na kutumbuiza kesho Ijumaa ambapo baada ya kutumbuiza atatembelea vituo kadhaa vya watoto yatima hapa jijini Dar es Salaam ataanza na kituo cha Trust youth Care pia mesema kuwa kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 10 kwa kabla ya saa sita usiku na baada ya saa sita kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 15 atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam. Nyimbo atakazo tumbuiza ni WekaWeka Kutibu pamoja na Dalia.
Kulia ni Meneja mauzo wa kinywaji cha Johnnie worker, Francis Tibaikana akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vinjwaji vitakavyokuwepo wakati wa msanii Frasha akitumbuiza amesema kuwa chupa moja ya kinjwaji cha Johnnnie Worker itauzwa kwa shilingi laki moja na elfu idhirini badala ya shilingi laki moja na elfu hamsini. Pia aliwaalika watanzania kuhudhulia wakati wa msanii huyo akitumbuiza na kujipatia ofa za pumbuzo la bei la kinywaji cha Johnnie Worker ikiwa msanii huyo atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...