BJ and Hellen Mwakyoma (Gwantwa) Wa Chicago-IL anasikitika kutangaza kifo cha Mama yao Mama Tamali Mwakyoma, Kilichotokea nchini India juzi October 17, 2015 alikokwenda kwa matibabu. Habari ziwafikie Ndugu jamaaa na Marafiki Popote Pale walipo.
BJ na Hellen wanatarajia kuondoka Marekani Jumanne kurudi Tanzania kwa Mazishi, ambapo shughuli za awali za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es salaam, nyuma ya jengo la Kamisheni ya Vyuo Vikuu barabara ya Rose Garden.
Kwa pole na salaam za rambi rambi
mnaweza kuwasiliana na Gwantwa @ 773-262-2703
Bwana ametwaa, na Bwana Ametoa,
Jina la Bwana na Lihimidiwe.
AMINA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...