KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI (PRESS RELEASE)
Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL unachukua fursa
hii kuwaarifu abiria wa treni ya deluxe ya Jumapili Oktoba 25, 2015
kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kuwa
muda wa kuondoka umesogezwa mbele kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku wa siku hiyohiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo uamuzi huo umechukuliwa maalum ili kuwapa fursa Abiria
waliojiandikisha kupiga kura kutumia haki yao ya kikatiba kikamilifu.
Utaratibu
huu utatumika pia kwa treni kwa siku hiyo zitakazokuwa zinaanza safari zake
kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam nazo zitaanza safari hizo saa 2
usiku.
Wito
unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.
Shime
kila Mtanzania ajitokeze kwenda kutumia
haki yake ya kikatiba kwa kumchagua Kiongozi mwenye sera anayoiafiki.
Imetolewa
na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
Dar
es Salaam,
Oktoba
21, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...