SHANGWE za muziki mnene wa 93.7 EFM ,kwa mara nyingine tena ziliendelea  ndani ya bagamoyo . Burudani ya aina yake  ikiongozwa na timu nzima ya EFM ilishushwa ndani ya mageti mia Adon lodge. Wakazi wa bagamoyo walipata nafasi ya kukutana na watangazaji, na RDJ’s huku  wakifurahia burudani ya pamoja.

Muziki mnene bar kwa bar ulipambwa na kabumbu kati ya EFM na Bagamoyo veterani ambapo Bagamoyo veteran waliibuka na ushindi wa bao moja huku EFM wakiambulia sifuri.

Tangu kuanza kwa mechi hizi hii ni mara ya pili kwa 93.7 EFM kufungwa,mara ya kwanza ilifungwa bao mbili na buffalo fc ya kisarawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...