SHANGWE za muziki mnene wa 93.7 EFM bado zinaendele. Ijumaa iliyopita ilikuwa zamu ya wakazi wa Tegeta . Burudani ya aina yake ikiongozwa na timu nzima ya EFM ilishushwa ndani ya kimori high way park Tegeta , huku wakazi wa Tegeta wakikutana ana kwa ana na watangazaji na RDJ’s wa 93.7EFM. 
Burudani ilianza na kabumbu kati ya EFM na Boko beach veteran katika uwanja wa boko beach ambapo EFM waliibuka na ushindi mabao matatu huku Boko beach veteran wakiambulia sifuri. 
"Muziki mnene bado unaendelea, nawaambia wasikilizaji wetu ambao hatujawafikia wawe wavumilivu na wajiandae kwa kuwa tutawafikia kuwapatia burudani ya aina yake", alisema Dennis Ssebo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano wa EFM, ambaye pia ni kocha mchezaji.
 Wafanyakazi wa 93.7 EFM walivyojumuika na mashabiki uwanjani kushuhudia mechi kati ya EFM na Boko Beach veteran.
 Timu za 93.7 EFM na Boko Beach veteran katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza.
 Mashabiki waliojitokeza uwanjani kushudia mtanange huo mkali.
 Nyomi ya wakaazi wa Tegeta walivyojitokeza kula Muziki Mnene ndani ya Kimori Highway Park Tegeta baada ya gemu. Palikuwa hapatoshi!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...