THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Natu Rashid Msuya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi, Oktoba 29, 2015 Ikulu, Dar es Salaam na Katibu Mkuu - Ikulu, Ndugu Peter Ilomo uteuzi huo ulianza Jumapili ya Oktoba 25 mwaka huu, 2015 na ni wa miaka mitatu.
Bibi Natu Msuya ni Mshauri wa Wanafunzi, Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE cha Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Oktoba, 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...