Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas (wapili kulia) akimkabidhi jezi Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey-Wanawake – Kidawa Abdallah (watatu kushoto) leo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo NMB ilitangaza udhamini wake kwa Timu ya Taifa ya Hockey inayotarajiwa kushiriki mashindano ya Afrika kuwania kufuzu mashindano ya Olimpiki (Olympic Qualifier) mashindano yatakayoanza Oktoba 23 mwaka huu. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo – Juliana Soda na Kocha wa Timu ya Taifa ya Hockey – Wanawake – Valentina Quaranta (kulia).
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas (wapili kulia) akimkabidhi jezi Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey-Wanaume – Amarjeet Ruprai.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo – Juliana Yasoda (Wapili kushoto) akikabidhi bendera ya taifa kwa Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey
Kocha wa Timu ya Taifa ya Hockey – Wanawake – Valentina Quaranta (kulia) akitoa shukurani kwa NMB kwa niaba ya Timu ya Taifa ya Hockey.
NMB YADHAMIRIA KUINUA WANAWAKE KUPITIA MICHEZO
NMB YADHAMIRIA KUINUA WANAWAKE KUPITIA MICHEZO
Benki ya NMB imeidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa
Hockey katika mashindano ya Africa Olympic Qualifier yatakayofanyika kuanzia
Oktoba 23, 2015 mpaka Novemba 1, 2015 – Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa na lengo
la kuinua maisha ya wanawake kupitia michezo.
Udhamini huo ni pamoja na kutoa tiketi za ndege kwa
wachezaji wote na viongozi pamoja na vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mavazi
ya safari kwenda Afrika ya Kusini vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni
17.
Afisa wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas alisema
benki ya NMB marazote hufarijika inapopata nafasi ya kusaidia michezo kwani kwa
kufanya hivyo inaonyesha kujali kwao kwani miongoni mwa wapenda michezo na
wachezaji wenyewe, ni wateja wa NMB.
“Tunaamini
michezo ni muhimu katika kubadilisha maisha ya wachezaji ambao wengi wao ni
vijana, hivyo udhamini wetu kwa Timu ya Taifa ya mchezo wa Hockey Tanzania utaongeza
chachu ya ushindi kwa mchezo ambao unaonekana mgeni Tanzania, tunaamini mchezo
huu pia utatoa fursa kwa vijana kupata ajira pamoja na kuitangaza nchi yetu
kupitia michezo ya Olimpiki.” Alisema Bwana Barnabas
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...