Na Lorietha Laurence - Maelezo.
JESHI la Polisi nchini kwa
kushirikiana na Ofisi za Shirikisho la Polisi Duniani (Interpol) kanda ya Kusini mwa Afrika, imefanikiwa kukamata nyara za serikali zenye thamani ya Tsh.
Milioni 81 na watuhumiwa 121 wa makosa mbalimbali.
Akizungumza na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi (Oktoba 1, 2015), Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi, Kamishna Diwani Athuman (pichani), alisema kuwa lengo la
operesheni hiyo ni kuongeza tija katika swala zima la kupambana na uhalifu.
“Lengo la operesheni
hii ni kuongeza tija katika kupambana na hali ya uhalifu na kuweka mazingira
salama kwa wananchi na nchi jirani” alisema Kamishina Athuman.
Aidha aliongeza kuwa operesheni hiyo ilifanyika nchi nzima katika kanda nane ikiwemo kanda ya Kaskazini, kanda ya juu
Kusini, kanda ya ziwa, kanda ya magharibi, kanda ya Zanzibar, kanda ya kati na
kanda ya kusini na kufanikiwa kukamata
vielelezo na watuhumiwa wa makosa mbalimbali.
Kamishani Athumani
alisema kuwa vielelezo vilivyokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na magari
mawili yaliyoripotiwa kuibiwa nchini Japan na Afrika ya kusini ,dawa za
kulevya, wahamihaji haramu 7, kutoka Kenya, Burundi na Msumbiji, bidhaa
zilizopigwa marufuku zenye thamani ya Tsh. Milioni 3.5 na madini yenye thamani ya Tsh. Milioni 74.
Aliongeza kuwa watuhumiwa
mbalimbali walikamatwa kwa kujihusisha na makosa ya kuhujumu miundo mbinu ya Shirika
la Umeme Nchini (Tanesco) na hatua za kisheria zitachukuliwa endapo watakutwa
na hatia na kufikishwa mahakamani
Kamishina Athumani
amewaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pale wanapoona tukio la
uhalifu kutoka kwa mtu au kundi la watu
likiingia nchini kinyume na sheria na pia kuwa makini wakati wanapoagiza
magari kutoka nje kwa kuwasiliana na
ofisi za Interpol za ndani na nchi husika ili kuepuka usumbufu wa kukamatwa na
gari za wizi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...