GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Professa Benno Ndulu (Pichani), ameshinda tuzo
ya ‘Gavana Bora wa Afrika kwa mwaka 2015.
Tuzo
hiyo inayojulikana kama ‘Central Bank Governor of the Year’ ilitolewa na
taasisi ya Africa Investor (Ai) jijini New York, Marekani hivi karibuni katika
mkutano wake wa nane uliohudhuriwa na zaidi watu 250 maarufu katika biashara,
serikali, maendeleo, sekta ya fedha na wakuu wa nchi tano za Afrika.
Prof.
Ndulu aliibuka kidedea kwa kuwashinda magavana wa benki kuu 10 zingine za
Afrika za Afrika Kusini, Uganda, Botswana, Sierra Leone, Rwanda, Nigeria,
Namibia, Misri na gavana wa Benki Kuu ya nchi za Afrika ya Kati inahudumia nchi
sita za Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Guinea ya Ikweta, Gabon na
Jamhuri ya Congo.
Ai
ni taasisi inayoongoza ya uwekezaji na mawasiliano barani Afrika ambayo
inawaleta pamoja wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani wenye vitega
uchumi vyao barani Afrika.
Vigezo
viliyotumika kumpata gavana bora wa mwaka wa Afrika ni umahiri katika eneo la kazi
na kuonesha jinsi umahiri huo ulivyonufaisha sekta ya uwekezaji katika nchi
husika na mchango wa magavana katika kuendeleza mazingira wezeshi kwa
wawekezaji wa ndani na kikanda (sub-region).
Vingine
ni mchango wa magavana katika kukuza uchumi na maendeleo endelevu ya nchi zao
na nafasi zao katika kukuza mtazamo wa Afrika kama kituo bora cha kupokea
vitega uchumi.
Katika
taarifa yake ya ushindi, Ai ilimpongeza Gavana Ndulu kwa ushindi katika
kipengele hicho cha Gavana Bora wa mwaka barani Afrika.
“Mafanikio
yako bila shaka yataendelea kutoa hamasa na kivutio kwa viongozi wakuu wa
serikali na sekta ya biashara wanaofanya juhudi za kuikuza taswira ya sekta ya
uwekezaji barani Afrika,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Ai.
Hii
ni mara ya pili kwa Profesa Ndulu kushinda tuzo ya kimataifa tangu alipoteuliwa
kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2008. Mwaka 2009, jarida maarufu la
Emerging Markets linalochapishwa jijini London, Uingereza, lilimtangaza Profesa
Ndulu kuwa ‘Gavana Bora wa Bara la Afrika kwa mwaka huo. Jarida hilo hutambua
mafanikio yanayofanywa na watendaji wakuu wa benki kuu na mawaziri wa fedha na
kuwapa tuzo wakati wa mikutano ya Benki Kuu ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha
la Kimataifa (IMF) inayofanyika kila mwaka.
Imetolewa
na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na
Itifaki
Oktoba
12, 2015
Ni kumpongeza Gavana kwa tuzo hii aendeleze kazi nzuri.
ReplyDeleteHongera kabisa, kila jamii na taifa lina wakati wake wa rising and shining duniani katika nyanja mbali mbali na kuna dalili zote kwamba Tanzania na watanzania wakati umefika wa kutambulika na kutangazika katika kupiga hatua ya maendeleo ya kweli katika fani mbali mbali ikiwa kwenye uchumi, siasa, taaluma, michezo au burudani kwa kweli inatia moyo sana.
ReplyDelete