Meneja wa Mfuko wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akiwaongoza wanachama wapya waliojiunga na mpango huo, wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha maafisa na mabalozi wa PSPF, na wanakikundi wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, (VOWET), kwenye ukumbi wa Belmonte jijini Dar es Salaam, Oktoba 13, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

Na K-VIS MEDIA


MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezidi k”kupenya’ kwenye sekta binafsi na kuvuna wanachama zaidi kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, ambapo wanakikundi wajasiriamali wa kundi la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Voice of Women Entrepreneurs Tanzania-VOWET).

Wanachama hao wapya walijiunga baada ya kushiriki warsha ya siku moja ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jingo la makao makuu ya PSPF, jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2015, ambapo Mabalozi wa Mfuko huo, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto na Mwanamitindo wa Kimataifa anayeishi na kufanyia kazi zake jijini New York Marekani, Flaviana Matata, walishiriki kutoa “Darasa” kuhusu umuhimu wa Watanzania walio katika sekta bionafsi kuchangamkia fursa kupitia kuiunga na uamancaha wa Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.

Mabalozi hao waliongozwa na Meneja wa Mpango wa PSS, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Magire Werema, ambao wote kwa pamoja walifafanua na kueleza kwa kina faida za kuwa mwanachama wa Mfuko huo, ambapo kwa muda mfupi baada ya kujiunga Mwanachama anawezakufaidi mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko huo ikiwemo mikopo ya nyumba, Fao la Elimu, na mengine mengi.
Kufuatia :Darasa” hilo, wanachama wa VOWET walijiunga na Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.
 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, akitoa mada.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...