THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax:
255-22-2113425
|
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
amemshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi na busara zake wakati nchi
hiyo ilipoingia kwenye machafuko ya kisiasa mwaka 2007.
Rais Kenyatta amemshukuru Rais
Kikwete leo mbele ya wafanya biashara wa Kenya na Tanzania, wakati wakufungua
Kikao cha wafanyabiashara pamoja jijini Nairobi leo asubuhi.
"Kama isingekua msaada wako
mwaka 2007 na juhudi zako, historia ya Kenya leo ingekua tofauti, asante kwa
msaada wako na tunautambua urafiki wetu". Rais Kenyatta amemuambia Rais Kikwete.
Kenya iliingia kwenye machafuko ya
Kisiasa mwaka 2007 kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo ambapo mapigano na
machafuko yalisababisha vifo, uharibifu wa mali na watu kukosa pahali pa kuishi
na kusababisha kukimbia makazi yao.
Rais Kikwete aliombwa na Umoja wa
Afrika kama mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusaidia katika juhudi za
usuluhishi ambapo hatimaye, pande mbili zilizokua zinazozana ziliunda serikali
ya Umoja wa Kitaifa ambayo ilileta utulivu na kusitisha mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe.
Rais Kenyatta pia amemshukuru Rais
Kikwete kwa juhudi zake kwenye uwekezaji na kwenye miundombinu ambayo
inaimarisha Jumuiya.
Rais Kenyatta pia ametambua na
kupongeza juhudi za Rais Kikwete katika kuhamasisha uwekezaji, biashara,
miundombinu na uwekezaji kwa ujumla na kueleza kuwa katika kipindi cha miaka 10
ya Rais Kikwete biashara na mauzo ya Kenya Tanzania yameongezeka kwa asilimia
5.5 katika kipindi hicho.
Nae Rais Kikwete amesema anaamini
biashara na uwekezaji baina ya Kenya na Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla
bado unaweza kuongezeka mara tatu zaidi ya sasa.
Rais Kikwete pia ametembelea makao
makuu ya jiji la Nairobi na kupokelewa na gavana wa Nairobi Dr. Evans Kidero
ambapo amekabidhiwa ufunguo wa jiji la Nairobi na pia kupata heshima ya
kuzindua mtaa ulioko maeneo ya Ikulu ambao umepewa jina la Jakaya Kikwete. Mtaa
huo ulikua unajulikana kama barabara ya Milimani.
Kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete
kuzindua barabara hiyo Dr. Kidero amesema Kenya inamshukuru Rais Kikwete kwa
dhati na kwamba Ushirikiano wa kibiashara na kijamii ni mzuri sana.
Rais Kikwete anatarajia kuhutubia
Bunge la Kenya baadae mchana na kuwaeleza wananchi wote wa Kenya kuwa
anatarajia kukabidhi madaraka kwa Rais Mwingine baadae mwaka huu.
Imetolewa
na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa Rais, Msaidizi,
Nairobi-Kenya
6 Oktoba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...