THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi katika Mahakama kama ifuatavyo;
Rais amemteua Bi. Katarina Revocati kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (Chief
Registrar). Kabla ya uteuzi huu, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama ya
Rufani.
Rais pia amemteua Ndugu
John Rugalema Kahyoza kuwa Msajili
wa Mahakama ya Rufani na kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kahyoza alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
Mwingine
aliyeteuliwa ni Ndugu Ilvin Claud Mugeta
ambaye anakuwa Msajili wa Mahakama Kuu. Kabla
ya Uteuzi huu ndugu Mugeta alikua Mkurugenzi wa Ukaguzi na Maadili.
Uteuzi huu
umeanza tarehe 3 Oktoba, 2015.
Imetolewa na:
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
19
Oktoba, 2015.
Hongera sana Mh. Katarina Revocati, MUNGU akubariki sana, natumaini wewe ndiye utakuwa jaji mkuu mwanamke wa kwanza kwa Tanzania, ubarikiwe sana.
ReplyDeleteMimi nimefurahi sana kwa jinsi MUNGU anavyokupaisha siku baada ya siku. Nakukumbuka sana wakati ukianza kazi RM, Mbeya, wakati huo ukiwa binti mdogo.
BWANA YESU AKUBARIKI SANA MHESHIMIWA.