THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa,
Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbalimbali.
Aidha,
Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala
wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa mujibu
wa uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari
Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha,
kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi na Ndugu Zidikheri Mgaya Mundeme
kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wengine
walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel
Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Walioteuliwa
kuwa Makatibu Tawala wa Mikoani Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa
wa Katavi.
Katibu Mkuu
ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Naibu Makatibu
Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda
kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wateuliwa
hao wote wataapishwa asubuhi ya Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es
Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
24 Oktoba, 2015
Duh.. Lol
ReplyDelete