Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi (Anayehojiwa na waandishi wa habari pichani)ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo Emmaneul Makaidi aliyefariki Dunia jana mkoani Lindi.
Katika salam zake, Malinzi amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja na wadau wa mpira wa miguu nchini, kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
Marehemu Emmanuel Makaidi alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba 1960-1970 katika nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi, Katibu Mkuu na kukaimu Uenyekiti wa klabu ya Simba kabla ya kujiunga na masuala ya kisiasa.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini na watanzania, TFF inawapa pole wafiwa na kuwatakia faraja katika kipindi hichi cha maombelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...