Naibu Mkurugenzi mkuu wa benki M Bi Jacqueline Woiso akitoa
ripoti ya fedha ya benki hiyo katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu wa
2015 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt
Regency hii leo. kushoto kwake ni mkurugenzi wa mawasiliano wa benki hiyo bw.
Allan Msalilwa
BENKI M leo hii imetangaza ripoti yake ya fedha katika kipindi cha robo ya tatu ya
mwaka huu wa 2015, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika
hoteli ya Hyatt Regency leo hii.
Akizungumza
katika mkutano huo, Naibu mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso
alisema kuwa kwa upande wa rasilimali, mizania ya benki imeendelea kukua kwa
asilimia 19% kufikia bilioni 823.43 bilioni katika robo ya tatu ya mwaka 2015,
kutoka sh 689 bilioni za mwezi December 2014. Hiki ndio kipimo cha ukubwa wa
benki au taasisi yoyote ya kifedha (
Balance sheet size).
Bi Woiso
aliendelea kusema kuwa “amana za wateja pia zimeongezeka kufikia 696.22 Bilioni,
ni ongezeko la asilimia 19% kutoka December 2014. Hii inadhihirisha imani kubwa
iliyojengwa na jamii kwa ujumla”.
Pia
mikopo katika sekta za uchumi, sehemu kubwa ya mikopo iliyotolewa na benki hiyo
kipindi cha robo mwaka huu ni katika sekta ya Kilimo, uzalishaji viwandani, biashara,
Utalii pamoja na sekta ya Ujenzi na makazi. Pamoja na ongezeko hilo benki hiyo
imeendelea kuwa na asilimia ndogo sana ya mikopo isiyozalisha faida ambayo ni
asilimia 2.6% ya jumla ya mikopo yao.
“Faida kabla ya kodi (Profit Before Taxes) imeongezeka
kwa asilimia 32% kufikia sh 17.34
bilioni kutoka sh 13.12 bilioni September mwaka 2014. Ongezeko hili
limechangiwa zaidi na ongezeko lilitokana na mapato yasiyotokana na riba. Faida
katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka jana ilikiuwa ni sh.15.09 bilioni na hivi
sasa ni sh.16.25 Bilioni.
Mafanikio yetu yanatokana na ufanisi mkubwa katika
teknologia tunayotumia katika kufanya miamala mbali mbali pamoja na bidhaa na
huduma zenye ubora wa hali ya juu katika soko la kibenki nchini”. alisema Bi
Woiso.
Aliongeza
kuwa katika kipi hicho cha robo ya
tatu ya mwaka 2015, zipo changamoto kubwa zilizojitokeza kama vile uhaba wa
fedha katika soko la ndani la kifedha (domestic market) na kusababisha viwango
vya riba kuongezeka kwa takriban asilimia 5.
“Vile
thamani ya shilingi iliendelea kuporomoka kutoka viwango vya dola 1/sh 2,000
hadi kufikia dola 1/sh.2,200. Athari za kushuka thamani ya sarafu yetu ni kubwa
hususan kwa nchi kama Tanzania ambayo uchumi wetu unategemea bidhaa za nje kwa
kiwango kikubwa sana, pia gharama za maisha zinaongezeka kwa jamii kwa ujumla”,
alimalizia Bi. Woiso.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...