Kutoka Kushoto - Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt.
James Mataragio, Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, Katibu Mkuu Wizara ya
Maendeleo ya Nishati na Madini (Uganda), Dkt. Fred Kabagambe Kaliisa na Meneja
Mkuu wa Total E&P Uganda, Ndg. Adewale Fayemi wakipongezana baada ya kutia
saini Hati ya Makubaliano (MoU) baina ya Serikali ya Uganda na Tanzania juu ya
utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda
(Kabaale) mpaka bandari ya Tanga (Tanzania).
SHIRIKA
LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC)
|
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Jamhuri ya Uganda, TPDC na Total E&P Uganda wametia saini Hati
ya Makubaliano juu ya utekelezaji wa mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka
Uganda kupitia Tanzania.
Hati hii ya Makubaliano inafungua
fursa kwa Serikali hizi mbili kufanya kazi kwa pamoja kuangalia uwezekano wa
kuendeleza mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Kabaale Uganda kupitia
Tanzania mpaka bandari ya Tanga. Makubaliano haya pia yanatambua faida zaidi
zitakazopatikana kwa Tanzania na Uganda ambazo ni zaidi ya utekelezaji wa mradi
huu. Vilevile makubaliano haya yanatoa muongozo kwa pande zote zinazohusika
kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kuboresha tafiti zilizo kwisha fanyika juu ya
njia ya Tanga.
Akiongea baada ya kusaini hati hiyo,
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema
“Tanzania na Uganda wana historia ndefu ya ushirikiano na mradi huu utazidi
kuboresha ushirika kati ya nchi hizi”. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa
TPDC, Dkt. James Mataragio aliongeza kuwa, TPDC ina uzoefu wa muda mrefu katika
ujenzi, uendeshaji na utunzaji wa bomba na hivyo uzoefu huu utasaidia sana
katika utekelezaji wa mradi huu. Wiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alifungua rasmi mradi wa bomba la gesi la kilometa 542 kutoka Mtwara
kwenda Dar es Salaam unaomilikiwa na kuendeshwa na TPDC.
Imetolewa
na;
Mkurugenzi Mtendaji,
Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania,
S.L.P 2774,
Dar-es-Salaam.
Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...