Ibrahim Hassan Seushi
16 December 1948 – 25 July 2015
Familia ya Ibrahim
Hassan Seushi, kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru
ndugu, jamaa, majirani na marafiki wote waliofanikisha shughuli zote za msiba
wa Marehemu Ibrahim Hassan Seushi ambaye alifariki katika hospitali
ya Apollo, Chennai India tarehe 25 July
2015 na hatimaye kuzikwa tarehe 29 July 2015 Kituri,
Mwanga.
Shukrani za pekee
tunaomba ziwafikie wauguzi wa hospitali ya Muhimbili na Apollo, Eliamani
Seushi, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumhudumia, kwa sala, maombi na kujitokeza
kwenu katika kutufariji na kututia nguvu.
Kwa kuwa ni vigumu
kumshukuru kila mtu kipekee, tunaomba shukrani ziwafikie wote mliohusika kwa
njia moja ama nyingine. Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi MUNGU
awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.
Pumzika kwa Amani,
Mpendwa wetu, Baba yetu, Nguzo yetu.
Inna
Lillahi wa inna ilayhi Raji un – Hakika, sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika
kwake tutarejea - Quran 2:156
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...