OFISI Usambazaji na Ugavi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Eliud Njaila akiwaonyesha waandishi wa habari vizimba vya kupigia kura siku ya uchaguzi. 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wapiga kura waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika nchini kote siku ya Jumapili.

Akizungumza katika mkutano wa vyama vya siasa na NEC mjini Dodoma leo, Ofisa Mwandamizi wa tume hiyo William Kitebi, amesema watu hao hawataruhusiwa hata kama majina na taarifa zao zipo kwenye Daftari la Wapiga Kura (BVR).

“Hakuna jinsi ya kuwasaidia watu waliopoteza kadi zao za kupigia kura ,”amesema Kitebi
Hata hivyo, Kitebi amesema kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye BVR  kuna baadhi ya mambo NEC wameyawekea utaratibu ili watu waweze kupiga kura.

Amesema watu ambao namba za kadi zinatofautiana na zile zilizopo kwenye BVR  lakini taarifa nyingine ni sahihi wataruhusiwa kupiga kura.

“Kuna wale ambao picha zao hazionekani kwenye daftari lakini kadi za kupiga kura wanazo, hawa wataruhusiwa kupiga kura,”amesema.
Kuhusu wale wapiga kura walioathiriwa na mipaka ya utawala, Kitebi amesema maamuzi ya tume kuwa watu hao watapiga kura kwenye kata walizopo.

“Kuna maeneo kulikuwa na mabadiliko ya mipaka ya kiutawala baada ya zoezi la uandikishaji kama Kishapu (Shinyanga) na Kaliuwa (Tabora), wao wataruhusiwa kupiga kura kwenye maeneo yao mapya,”amesema.

Kwa upande wa wapiga kura ambao wanakadi za kupigia kura lakini hawaonekani kwenye BVR, Kitebi amesema hao wamewekewa utaratibu utakaowawezesha kupiga kura.


“Kama kule Mbarali (Mkoa wa Mbeya), kuna watu kama 6,000 ambao hawaonekani katika daftari lakini wanakadi na fomu zao zimejazwa na kuwasilishwa tume  hawa wanaruhusiwa kupiga kura,”amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...