JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

PRESS RELEASE 05/10/2015
MAJAMBAZI SUGU SITA WALIOMMUA AFISA WA POLISI ASP ELIBARIKI PALLANGYO WAKATWA. WAPATIKANA NA SILAHA MBILI.

WATUHUMIWA WA UGAIDI WAZIDI KUKAMATWA KATIKA OPARESHENI KALI INAYOENDELEA. SABA WASHIKILIWA POLISI KANDA MAALUM. PIA ZIMEKAMATWA BUNDUKI NNE NA RISASI 18
jeshi la Polisi kanda maalum ya dar es salaam wamefanikiwa kuwakamatwa majambazi sugu sita walioshiriki katika mauaji ya ASP Elibariki Palangyo huko nyumbani kwake Yombo Makangarawe tarehe 04.08.2015.
waliokamatwa ni: 1) OMARY SALEHE@BONGE MZITO (39) MKazi wa Mtoni mtongani ambaye ni Kiongozi wa kundi hilo
2) SAIDI SAIDI MAZINGE (37) Mkazi wa Tegeta Kibaoni
 3) RASHIDIWATSONB@ DODO(21) MKAZI WA Vingunguti
4)RAMADHANI SALUM@NGUZO 38 mkazi MBAGALLA KIBURUGWA
5) BAKARI SALIM RASHIDI@ MALENDA (38) Mkazi wa Mbagala kizuiani
6) HAMISI HAMISI @ FREEMASON 24 Mkazi wa Mbezi Mwisho
Afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi la Polisi alikuwa anafanya kazi Mkoani Morogoro katika kikosi Maalum cha kupambana na majambazi aliyekuja nyumbani kwake Dar Es salaam. Alikuja DSM kwa ajili ya kusalimia familia na ndipo alipovamiwa na majambazi usiku wa manane wakati amelala na familia yake.

Aidha mtuhumiwa  namba mmoja alikutwa na silaha bastola aina ya revolver iliyofutwa namba na baada ya mahojiano. aidha mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu kabla ya kufariki alijaribu kuwatoraka askari kwa kukimbia alijeruhiwa na hatimaye alifia njiani wakati akipelekwa hosptalini.

 Pia inasemekana marehemu alipotezana na familia yake miaka mitani iliyopita akiwa kwenye harakati ya ujambazi. Pia bonge mzito alikuwa akitafatwa na Polisi kwa matukio mazito ya ujambazi wa kutumia silaha na mauaji ambaye pia amehusika katika mauaji ya afisa wa Polisi nyumbani kwake usiku wa manane na kumuua mbele ya familia yake ikishuhudia.
Pia mtuhumiwa RASHIDI WATSON@ DODO alikamatwa maeneo ya Vingunguti tarehe 01.10.2015 akiwa na silaha aina ya Shortgun ilikatwa mtutu na kutengenezwa kienyeji ikiwa na risasi nne na betri mbili zilizounganishwa kwa ajili ya kulipua baruti.
 Watuhumiwa wengine watano watapelekwa mahakamani baada ya kuperuzi  na kukamilika kwa upelelezi wa shauri hilo.

WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WANAOJIHUSISHA WANAOJIHUSISHA NA UGAIDI WAPATAO  SABA WAKAMTWA, SITA KATI YAO NI WAFIMILIA MOJA 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na mikoa ya jirani pamoja na vyombo vingine vya dola limeendelea kufanya oparesheni ya kuwatafuta na kisha kuwakamata wale wote wanaojihusisha na matukio ya kupanga na kuvamia vituo vya Polisi, kuua askari/raia kisha kupora silaha jambo linaloashiria vitendo vya kigaidi. 

Oparesheni hii ni kali na ya aina yake kwa madhumuni ya kukomesha kabisa vitendo vya uvamizi wa vituo vya Polisi na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine lazima wakamatwe ili sheria uchukue mkondom wake. Oparesheni hii pia ina lengo la kuwaondolea hofu wananchi dhidi ya vitendo vya kigaidi nchini na kwamba wananchi waendelee kutoa taarifa juu ya watu kama hao ili nchi yetu iendelee kuwa na amani na utulivu. Majina ya watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
1. SIAD S/O MOHAMED ULATULE @ USO WA SIMBA, Miaka 67, Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga mkoa wa Pwani.
2. RAMADHANI S/O ALLY NGANDE, Miaka 29, Dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Kongowe.
3. HAMIS S/O MOHAMED SALUM SIMBA ULATULE, Miaka 51, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani.
4. ALLY S/O MOHAMED SALUM SIMBA ULATULE, Miaka 65, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani. 
5. NASSORO S/O SELEMAN ULATULE, Miaka 40, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani.
6. SELEMAN S/O ABDALLAH SALUM ULATULE, Miaka 83, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani.
7. SAID S/O ABDULLAH CHAMBETA @ Mzee wa Fasta, Miaka 40, Mfanyabiashara wa Mitumba, Mkazi wa Yombo Makangarawe. Mtuhumiwa namba 1,3,4 na 5 ni wa familia moja inayojihusisha na vitendo vya ujambazi pamoja na  vya kigaidi.
Tunawashukuru sana watanzania wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yao kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali ambao umesaidia kupata mafanikio yote haya. Tunawaomba waendelee kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kuendelea kutoa taarifa ili oparesheni hii iwe yenye ufanisi zaidi.

KUKAMATWA KWA BUNDUKI SMG MOJA NA SHORTGUN MBILI, BASTOLA MOJA PAMOJA NA RISASI 14.  
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa MUSSA S/O MALAKI AKUTI, Miaka 30, fundi wa magari, Mkazi wa Mbagala Charambe kwa kukutwa na bunduki aina ya “Chinese 56 SMG” yenye namba 563845189 ikiwa na magazine moja na risasi 14. Mtuhumiwa huyu alikamatwa tarehe 28/09/2015 maeneo ya Mbagala Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam baada ya Polisi kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

Bunduki hiyo ambayo aliiweka chini ya kiti cha pikipiki aina ya BOXER yenye namba T269 AUX inayosemekana kutumika katika matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Upelelezi unaendelea ili kuwakamata watuhumiwa wengine ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kutokana na tuhuma zinazowakabili. 

Katika muendelezo wa kuwasaka washirika wa MUSSA  MALAKI, alikamatwa mtu mmoja kwa jina la AMON @ MTU MFUPI na simu yake ilianza kufuatilia ndipo wenzake walimpigia simu wakimtaka wakutane maeneo ya Tabata ili wakapore fedha kule Sinza Bigbon. 

Askari walienda na mtuhumiwa maeneo ya Tabata na kuanza kuwafuatilia hao majambazi. Majambazi waliposhtukia mtego huo walianza kurushiana risasi ndipo jambazi mmoja alipigwa risasi na kufariki palepale. Alipopekuliwa alikutwa na Bastola aina ya FATIN-43 yenye nambari T0620-10J00413. 

Ufuatiliaji uliendelea ndipo alipokamatwa  JOSEPH S/O WAMBURA aliyekuwa akimfuatilia mteja aliyekuwa anachukua fedha benki. JOSEPH ALipopekuliwa alikutwa na karatasi ya kuchukulia fedha benki (pay-in-slip). Mtuhumiwa alikiri kuwa hiyo mbinu wameitumia kwa muda mrefu kumbe dhumuni ni kuwaangalia watu wanaochukua fedha nyingi benki kisha yeye huwasiliana na wenzake ili wawapore fedha. 

Wakati huo huo, imekamatwa bunduki nyingine aina ya SHOTGUN/GOBOLE baada ya mtu mmoja aliyekuwa anafuatiliwa na polisi kushtukia mtego na kutupa fuko la kiroba alilokuwa kisha kutokomea kusikojulikana. Lilipopekuliwa fuko hilo ilikutwa bunduki hiyo inayoonekana ilifukiwa ardhini.

Bunduki hii ilikamatwa tarehe 28/09/2015 huko kijiji cha MKULIWINI, Kata ya Bupu Mkoani Pwani baada ya polisi kupata taarifa na kuweka mtego wa kumkamata mtuhumiwa. Bado msako wa kumtafuta unaendelea ili kubaini wapi alikuwa anaipeleka silaha hiyo na kwa dhamira gani.

Aidha, katika msako wa kuwakamata majambazi wa kutumia silaha mnamo tarehe 30/09/2015 huko Vingunguti nyumbani kwa mtuhumiwa JUMA S/O MALIMBIKA ilikamatwa silaha aina ya SHOTGUN iliyotengenezwa kienyeji (GOBORE) inayotumia risasi za shotgun. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa bunduki ilipelekwa hapo na mtuhumiwa aitwaye RASHID S/O WATSON, Miaka 28, Mkazi wa Vingunguti ambaye amekamatwa kwa mahojiano zaidi ili kuubaini mtandao wa majambazi hao kwa lengo moja tu la kuusambaratisha.


POLISI YAOKOA MALI ILIYOIBIWA YENYE THAMANI YA TSHS 159,000,000/=
Mnamo tarehe 16.06.2015 majira ya saa 02:00 usiku, huko barabara ya Nyerere Jeshi la polisi kanda maalum Dsm lilipokea taarifa toka kwa ndugu FORD s/o MUSHI (40) mkazi wa Sinza aligundua kuvunjiwa ghala analotumia kuhifadhia bidhaa mbalimbali za dukani zikiwemo Fridge piece 133, Home Theatre idadi 582, kabati za nguo  17, bidhaa zote zenye thamani ya Tsh 159,680,000/=

Aidha Polisi kwa ushirikiano na taarifa mbalimbali za kiintelijensia walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja anayefahamika kwa jina la ABAS s/o RAMADHANI(31) mfanyabiashara mkazi wa kiwalani(w)Temeke.
Baada ya mahojiano mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na baada ya upekuzi alikamatwa na bidhaa zote zilizoibiwa pia aliwataja watuhumiwa wengine alioshirikiana nao ambao ni ALLY s/o SELEMANI SALIMU(37) mfanyabiashara mkazi wa Yombo(w)Temeke ambaye naye alikiri na kueleza kuwa baada ya kuvunja ghala hilo bidhaa zote walienda kuhifadhi kwa mtu aitwaye RICHARD S/o MARIDADI maarufu kwa jina la MUDY MKINGA (34) mkazi wa Chamazi alipopekuliwa tarehe 01/10/2015 saa 06:45 aubuhi  katika nyumba ya kulala wageni itwayo MBILWA GUEST iliyoko Bugurunini Malapa ambapo vipo vyumba anavyovitumia kama ghala ndipo bidhaa zote zilizoibiwa zilipatikana pale. Watuhumiwa wote wanahojiwa na watapelekwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. 

MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kimeendesha oparesheni maalum kuaznia tarehe 15/09/2015 hadi  04/10/2015 ya kuzuia, kukamata na hatimaye kuwachukulia hatua madereva wazembe wanaendesha vyombo vya moto hivyo kukiuka sheria za usalama barabarani. 

Makosa mbalimbali yalifuatiliwa ikiwa ni pamoja na ubovu wa magari, kuzidisha abiria, kukatisha route, uendeshaji wa hatari, matumizi mabaya ya barabara, kutokuwa na leseni, pamoja na makosa mengineyo. Katika makosa hayo, madereva mbalimbali walionywa, na wengine walitozwa tozo kulingana na utaratibu wa kisheria na makosa yao.
Kutokana na tozo zilizotozwa zimekusanywa jumla ya fedha za kitanzania shilingi MILIONI MIA TANO TISINI NA MOJA, MIA SABA SABINI ELFU TU (TShs. 843,260,000/=).

Lengo la oparesheni hii ya kikosi cha usalama barabarani si kukusanya fedha bali ni kuwakumbusha madereva wote wanaotumia barabara kutii sheria za usalama barabarani bila shuruti. Tinawahimiza watumiaji wote wa barabara kuzingatia hili kwa vitendo.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...