JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Mkoa wa Dodoma
Anwani ya Simu REGCOM
Simu Nambari: 2324343/2324384
E-Mail No. ras@dodoma.go.tz
Fax No. +255 026 2320046
|
|
Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa,
S.L.P. 914,
DODOMA.
|
Ndugu wananchi wa Mkoa wa
Dodoma, tarehe 25 Oktoba, 2015 ni siku ya Uchaguzi Mkuu hapa nchini; ambapo,
Watanzania wale wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha, watapata fursa
na kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi mbalimbali wa nchi yetu, kuanzia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.
Maandalizi ya kufanikisha
zoezi la Uchaguzi Mkuu kwa Mkoa wa Dodoma yamekamilika. Hadi kufikia siku ya
leo tayari wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma
wameshapokea vifaa vyote vitakavyo tumika kwenye zoezi la uchaguzi. Hadi
tunavyozungumza sasa, vifaa hivyo vinapelekwa kwenye vituo vya kupigia kura.
Vilevile, wasimamizi wa uchaguzi
kwenye wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma wameshapokea fedha za kuendeshea
uchaguzi Mkuu. Aidha, Mafunzo kwa
watendaji wote watakaoshiriki katika zoezi la uchaguzi yanahitimishwa kwenye
wilaya za Dodoma.
Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kuandikisha jumla ya
wananchi 1,053,136 kuwa wapiga kura
sawa na asilimia 102.74 ya lengo, ambapo
lengo ilikuwa kuandikisha watu/wapiga kura 1,025,084,
Hivyo, natumia fursa hii kuwataka wale wote waliojiandikisha kupiga kura katika
Mkoa wa Dodoma, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili Oktoba 25.
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi na zoezi la kuhesabu kura litaanza saa 10:00 jioni. Natumia fursa hii kusisitiza mambo machache ya muhimu
kwenye zoezi la uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na
wadau mbalimbali wanaoshiriki Uchaguzi Mkuu kama ifuatavyo:
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...