Baada ya
mafanikio makubwa 2014, tamasha kubwa la muziki Karibu Music Festival
lifanyikalo kila mwaka limerudi tena mwaka huu kwa kishindo kikubwa Novemba hii tarehe 6,
7 na 8.
Tamasha la Karibu Music Festival hufanyika kwa mfululizo wa siku 3 na litafanyika kwenye viwanja vya
Mwakalinga Bagamoyo karibu kabisa na ufukwe wa bahari ya Hindi.
Mambo
mazuri kwenye tamasha hili ni mchanganyiko wa mziki, utamaduni , michezo mbali
mbali kutoka kwa wasanii mbali mbali watokao barani Asia, Ulaya , America na
Afrika.Moja ya
sababu ya kuanzishwa kwa tamasha hili ni kukuza na kutangaza mziki na utamaduni
wa Afrika kwa nchi zingine. Miziki yenye asili ya pop, rock, Reggae, Hip Hop
Jazz, country hupata umaarufu miongoni mwa wahudhuriaji.
Mwaka huu
watunzi na waimbaji watapata nafasi ya kuuza na kuoromote albam zao, pia
wachonga vinyago na wasanii wengine watapata fursa ya kuonyesha kazi zao nzuri
kwenye tamasha hili.
Kaymu
Tanzania inakupa nafasi nzuri ya kuhudhuria tamasha hili la kipekee kwani
tiketi zitauzwa kwa bei nafuu sana haijawai kutokea.
Kwa watu 50 wa kwanza watajipatia tiketi kwa Tsh 2,500 badala ya Tsh 5,000
Nunua tiketi yako kwa kubofya Kaymu.
Usisahau kumtaarifu na umpendae juu ya jambo hili jema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...