Familia ya Marehemu Cyprian Tarimo ya Ukonga, Mombasa Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Mama Judith Tarimo kilichotokea Oktoba 25,2015 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Ukonga-Mombasa jijini Dar es salaam na Rombo Mahida, Mkoani Kilimanjaro.
Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki wote wa ukoo wa Tarimo na Shayo, popote pale walipo.
Mwili wa marehemu unataraji kuagwa Oktoba 28, 2015 kabla ya kusafirishwa siku hiyohiyo kwenda Mahida Rombo kwa maziko Alhamisi Oktoba 29,2015.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,
JINA LA BWANA YESU LIHIMIDIWE AMEN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...