Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa MONUSCO, Bw. Martin Kobler akisisitiza jambo wakati wa mazugumzo yake na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako Manongi. Bw. Kobler alifika katika Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu, kuishukuru Tanzania kwa mchango wake wa ulinzi wa amani katika Mashariki ya DRC. Mchango ambao amesema umeleta tofauti kubwa.
"Tafadhali nifikishie salamu na shukrani zangu kwa Mhe. Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Waziri wa Ulinzi" maneno ya Bw. Martin Kobler kwa Balozi Manongi walipokuwa wakiagana baada ya mazungumzo yao mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi
Maalum, New York
USHIRIKI wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Misheni ya
kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa
katika Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo ( MONUSCO),
kumeelezwa kutoa mchango mkubwa katika kurejesha hali ya Amani na utulivu
katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya
nchi hiyo.
Hayo
yameelezwa mwishoni mwa wiki, na Mwakilishi
Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika
DRC na Mkuu wa MONUSCO Bw. Martin
Kobler, wakati alipofanya mazungumzo na
Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Bw. Kobler na ambaye
alitumia fursa hiyo kuaga na kuishukuru
Tanzania kwa ushiriki na
mchango wake, amesema, katika maeneo mengi ambayo walinzi wa Amani wa Tanzania
wanayalinda hali ya Amani imerejea kiasi
ambacho wananchi waliokimbia vita
wamerudi na kuendelea na shughuli zako za kila siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...