CHAMAcha
Madaktari wa michezo Tanzania (TASMA) kinatarajia kunogesha tamasha la ‘Kandanda
day’ kwa kufanya kliniki siku ya Oktoba 17,mwaka huu katika Viwanja vya TCC Chang’ombe,jijini
Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu
wa tamasha hilo,Mohamed Mkangara,alisema kwamba TASMA kwa kushirikiana na
kamati ya kandanda Day wameamua kufanya kliniki hiyo ya wazi ili kuwapa fursa
wadau wa michezo kupata mafunzo na kupima afya zao.
“Kamati ya
Kandanda day,imeona kuna haja ya kushirikiana na ndugu zetu wa TASMA,ili kutoa
elimu ya afya,kwa wadau wa michezo nchini ambao watapata fursa ya kupima afya
zao bure,na baadaye watapata burudani ya kuangalia burudani ya mechi kati ya
timu Dizo One na timu Ismail,”alisema
Mkangara na kuongeza:
“Kikubwa
tunawashukuru sana TASMA kwa kuitikia mwito wetu wa kushirikiana nasi katika
siku hiyo muhimu, hususan kwa wapenda soka nchini,halikadhalika wadhamini wetu
kampuni ya Bin Slum Tyres kwa kutusaidia zoezi hili la kliniki.”
Kwa upande
wa Katibu Mkuu wa TASMA, Dk. Nassoro Matuzya,alisema kwamba maandalizi yote
kuhusiana na clinic hiyo yanaendelea vizuri na ametoa mwito kwa wadau wa
michezo nchini hususan wa soka,kujumuika kwa wingi katika viwanja hivyo.
“Kwa upande
wetu tunawashukuru kamati ya Kandanda,kutujumuisha katika tamasha hilo kutoa
elimu pamoja na kutoa huduma ya upimaji afya kwa Watanzania wanamichezo na
wadau wa michezo nchini,kwa hiyo tunapenda kuwakaribisha wadau wajitokeze kwa
wingi katika siku hiyo,”alisema Matuzya.
Tamasha la
mwaka huu mbali na kiliniki pia kutakuwa na shughuli mbalimbali za soka na
burudani zikiendelea,ambazo zimepata kuongezewa nguvu na udhamini kutoka
kampuni ya matairi ya Binslum.SBS kupitia kinywaji chake cha Pepsi.Michuzi
Media group,Blogu ya Saleh Jembe.kampuni ya kutoa mikopo ya Bayport pamoja na
kampuni ya kuchapisha matangazo ya SDS.
Kiliniki
itaanza asubuhi saa mbili kamili kwa wadau wa michezo kupata mafunzo kutoka kwa
madaktari wa TASMA na kufuatiwa na michezo ya soka na burudani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...