Makamu Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid M. Hamid (wa pili kushoto) akisoma matokeo ya wagombea nafasi ya Urais leo jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,anayemfuata kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Mhe. Damian Lubuva na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mhe. Kailima Ramadhani
Baadhi ya waandishi wa Habari wa Ndani na Nje ya nchi wakifuatilia zoezi la kutangazwa kwa matokeo ya wagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Msaidizi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bw. Matson Chiizi akihojiwa na mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya Ujerumani (DW) Bi.Hawa Bihoga kuhusu namna gani analiona zoezi la utangazaji wa matokeo linafanyika.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wanne kushoto kwa waliyokaa katika picha ya pamoja kwa baadhi na waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi za Jumuiya ya SADC walipotembea ukumbi unaotumika kutangazia matokeo ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Edward Kondela akimhoji mmoja wa waangalizi wa uchaguzi ambaye ni Mwenyekiti wa SADC nchini Malawi Bw.Justice Mbendera alipotembelea ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais leo jijini Dar es Salaam. Picha na Anitha Jonas – MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...