Taswira za juu za usiku za Kituo cha michezo kwa vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK Youth Sports Centre) cha Kidongo Chekundu Dar es salaam. Kituo kitafunguliwa rasmi kwa umma tarehe 19 Oktoba mwaka huu. Uzinduzi utafanyika tarehe 17 Oktoba.
Hii ndiyo zawadi ambayo Rais Jakaya Mrisho Kikwete anawaachia Watanzania baada ya kuwa mtumishi wao kwa miaka 10, ambapo kupitia hapa vipaji vya vijana kwenye michezo mbalimbali vitagunduliwa na kuendelezwa. Mradi huu umefadhiliwa na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza cha Sunderland kwa kushirikiana na kampuni ya kuzalisha umeme ya SYMBION POWER.
Makocha wa kimatifa kutoka Uingereza na Marekani watahudumu katika kituo hiki, ambapo kocha wa soka atatoka Uingereza na kocha wa mpira wa kikapu atatoka NBA ya Marekani.
Wananchi wanaalikwa kutembelea kituo cha vijana JMK
siku ya Ijumaa,tarehe 16 Oktoba ili kupata vitambulisho vinavyovaliwa mkononi vitakavyowawezesha
kuhudhuria ufunguzi wa kituo tarehe 17 Oktoba.
Vitambulisho hivi ni vichache,
vitatoloewa kwa wale wachache watakaowahi kufika.
Siku ya Ijumaa tarehe 16 kuanzia saa tatu asubuhi;
watu wazima kwa watoto wanaweza kufika na kuchukua hivi vitambulisho kwenye
kituo kilichoko kwenye kona ya Mtaa wa Makamba karibu na Shule ya Sekondari ya
Manispaa mkabala na Rex Energy jijini Dar es Salaam.
Vitambulisho hivi
vitatolewa kama tiketi ya bure ya kumruhusu mhusika kuhudhuria shughuli ya
ufunguzi tarehe 17 Oktoba.
Jumla ya vitambulisho 1000 vitagawiwa kwa Wananchi,
shule zilizozunguka eneo hilo pamoja na ligi za michezo mbali mbali.
Wahudhuriaji wote WANAPASWA kuvaa hivi vitambulisho kwenye mikono yao ili
kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli ya ufunguzi tarehe 17. Viburudisho
kama vile maji, vitafunwa na barafu (ice cream) ambavyo vitatolewa na Kampuni
ya Azam.
Kituo kitafunguliwa tarehe 19 Oktoba
hatahivyo ili kuweza kutumia hicho; itampasa kila mtu kusajili maelezo mafupi
binafis. Wananchi waweza kupata fomu za kujisajili kwa kuzifuata kwenye kituo
kuanzia tarehe 16 Oktoba au kuzipakua kutoka wenye tovuti jmkpark.org au waweza
kututumia ombil la fomu kupitia info@jmkpark.org
.
Mara fomu itakapokuwa imejazwa, tafadhali tutumie kupitia info@jamkpark.org au ilete na kuiacha
kwenye nyumba ya mlinzi kwenye lango kuu la kituo liloko mtaa
wa Makamba mkabala na Hekalu la Singa Singa (Sikh Temple)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...