Katika kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum itakayoitwa “Kamati ya Taifa Stars” ambayo majukumu yake yatakua:
(i) Kuimarisha huduma kwa wachezaji,
(ii) Uhamasishaji na Masoko,
(iii) Kuhamasisha wachezaji,
(iv) Kuandaa na kusimamia mkakati wa Ushindi.

Kamati hii itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), Wajumbe ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.
Aidha Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu katika kutekeleza majukumu hayo.
Wadau wa mpira wa miguu ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu mbalimbali katika kamati hiyo wanaombwa waitikie wito huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safari hii kocha amefanya uteuzi wa wachezaji warefu na wenye maumbo lakini kuna tatizo la PUMZI.Wachezaji wanachoka haraka matokeo yake wanaanza kubutua mipira hovyo (bora liende).

    1.Kuna tatizo la kiungo wa kupenyeza pasi kwa wafungaji,atafutwe haraka kabla ya klukutana na Aljeria

    2.Kama kuna nafasi huyu kijana wa Yanga,Malimi Busungu aongezwe.

    3.Beki imekaa vizuri,washambuliaji wako vizuri.Tatizo liko midfield

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...