
Meneja Mkuu wa kampuni ya Tigo, Diego Gutierrez, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano kuhusina na kampuni ya Tigo kuanza kutumia mfumo wa kwanza Afrika wa mawasiliano ya 4G DVNO ikishirikiana na Uhuru One.

Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akiwa na Mwenyekiti wa uhuru One Rajab Katunda wakati wa uzinduzi kuanzisha kutumia mfumo wa kwanza Afrika wa mawasiliano ya 4G DVNO ikishirikiana na Uhuru One.
KAMPUNI ya Tigo na kampuni ya UhuruOne wameanzisha ushirikiano na kuunda mfumo wa utoajihuduma za kimtandao usiotumia miundombinu asilia ya mawasiliano (Data Virtual Network Operator – DVNO) na ambao utaiwezesha UhuruOne kupanua upatikanaji wa huduma zake kwa kutumia teknolojia ya 4G.
Aina hii ya mfumo wa mtandao ni ya kwanza barani Afrika.
Mfumo wa DVNO utaiwezesha UhuruOne kusambaza taarifa za kimtandao pamoja na mtandao wa data wa Tigo 4G LTE utakaowezesha wateja wake kutumia data zilizowezeshwa kupitia kasi kubwa ya 4G.
Akitoa maoni yake kuhusu hili, Meneja Mkuu wa Tigo, Gutierrez alisema: “Hii ni mara ya kwanza barani kuwepo na ushirikiano wa aina hii ambapo Tigo inafurahia kufanikisha jambo hili kwa kushirikiana na UhuruOne.
Kuzinduliwa kwa teknolojia ya 4G ni sehemu ya muendelezo wa mkakati wa Tigo kuboresha ubora huduma zake na kuwafikishia watu wengi zaidi huduma ya mawasiliano nchini.”
Aidha Mwenyekiti wa UhuruOne Rajabu Katunda alisema“tunaiona Afrika ikichipua kiteknolojia, lakini kujumuisha uwanda mpana wa mawasiliano na dijitali kwenye uchumi wetu kutautendea uchumi wetu jambo ambalo litatuneemesha sisi wenyewe na kutuinua kimaisha. Hili ni jambo la kipekee na la kujivunia kwa UhuruOne ambayo imekuwa katika harakati za ubunifu kupitia mtandao wa intaneti tangu mwaka 2009 na pia ni mwanachama mwasisi wa Umoja wa Dynamic Spectrum”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...