Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi iliyofanikisha upatikanaji wa Gari  la zimamoto, Mussa Bibose akitoa maelekezo kwa wananchi waliohudhuria shughuli ya kukabidhi gari hilo Kibada,Kigamboni  Jijini Dar es salaam. 

Mwenyekiti wa Umoja wa wananchi wa Kibada, Kigamboni Jijini Dar es salaam Bwana Lagano Mwampetu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari moja ya zimamoto iliyopatikana kwa Juhudi za umoja huo na kukabidhi kwa  Kamishna wa Operation Jeshi La Zimamoto na uokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali.

Kamishna wa Operation Jeshi La Zimamoto na uokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali akiangumza na wananchi waliojitokeza wakati wa kukabidhi Gari hilo ambapo amewapongeza wananchi wa Kibada kwa juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo katika maeneo yao.

Mwenyeikiti wa umoja wa wananchi wa Kibada, Kigamboni Jijini Dar es salaam Lugano Mwampeta akimpa maelekezo kamishna wa Operation jeshi la zimamoto na uaokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali wakati wa shughuli ya kumkabidhi gari moja la kuzima moto lililofanyiwa matengenezo kwa nguvu ya wananchi wa kibada kwa ajili ya kuwasaidia wakazi hao na majanga ya moto,makabidiano hayo yaliyofanyika Kigamboni Kibada Jijini Dar es salaam.

Gari la Jeshi la Polisi la zimamoto lilofanyiwa matengenezo na wananchi wa Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...