IMG_6436
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo hivi karibuni jijini Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MKURUGENZI Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Amon Manyama, alisema vita dhidi ya umaskini inakuwa na maana kubwa kama inalinganishwa na mazingira.

Alisema kwamba umaskini wa kipato ambao umekuwa ukipiganwa sana kwa sasa unastahili kupiganwa kwa kuangalia umaskini kutokana na ukweli kuwa kuboreshwa kwa mazingira ndio hatua kubwa ya kupigana na umaskini katika sura zote zilizobaki.

Mkurugenzi msaidizi huyo alisema hayo hivi karibuni mjini Mwanza wakati akielezea mradi wa mtaji na elimu wa UNDP ambao umefanyiwa kazi kwa pamoja kati ya shirika hilo, Tume ya Mipango, Hazina na Ofisi ya Makamu wa Rais, katika mafunzo ya siku moja ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, yaliyofanyika Mwanza.

Mradi huo umelenga kuwezesha ushirika wa akiba na mikopo katika wilaya sita nchini kuwezesha wananchi kushiriki katika kukabili umaskini unaosababishwa na mazingira.

Akifafanua alisema kwamba inawezekana muda wa kusubiri kuvuna samaki ziwani umekwisha kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika ni kupanda samaki ndani au nje ya ziwa na watu waweze kutumia nafasi hiyo kuboresha maisha yao.
IMG_6389
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumuni ya mafunzo hayo kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.

Alisema hali hiyo pia ipo katika misitu. Wakati watu wanakata misitu unawapa elimu na mtaji wa kupanda misitu mingine na hivyo mazingira yakaendelea kubaki na kuwa mtaji wa kukabili umaskini.

Mradi huo ambao upo katika wilaya sita kwa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2021 na ifikapo muda huo utakuwaupo wilaya 21 na kutumika kama kichochea cha utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu yenye nia ya kupiga vita umaskini, kuondoa ubaguzi na njaa.

Alisema mafunzo yaliyotolewa katika kongamano la viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika vya aina mbalimbali mjini Mwanza kwa msaada wa UNDP na kutekelezwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) yamelenga kuwezesha SACCOS kutambua fursa hizo za mazingira kukabili umaskini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...