Baadhi ya washiriki wa warsha iliyoandaliwa na UNESCO pamoja na Idara ya Mambo ya Kale wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mr Adelhelm Meru kufungua warsha hiyo iliyofanyika Coral Beach jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dr Adelhelm Meru akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Idara ya Mambo ya Kale kwaajili ya kujadili uboreshwaji wa utawala na matumizi endelevu ya hifadhi za urithi na mazingira za Tanzania, ambazo ni Magofu ya Kilwa; Michoro ya Asili Kondoa; Mji Mkongwe Zanzibar; Hifadhi ya Wanyama Selous; Hifadhi za Taifa za Serengeti, Ngorongoro, Lake Manyara na Mlima Kilimanjaro; na Hifadhi ya Mazingira ya Usambara Mashariki’.

Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
UNESCO kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya kale imeendesha warsha ya siku moja kwa wakuu wa hifadhi na vivutio vya utalii hapa nchini huku wakuu hao wakishirikishana mafanikio na changamoto zinazowakabili katika hifadhi zao.

Warsha hiyo iliyohudhuriwa na Wakuu wa hifadhi mbalimbali hapa nchini iliweza kuhusisha uwasilishaji wa mafanikio na changamoto wanazokutana nazo wakuu wa hifadhi hizo katika hifadhi huku matatizo makubwa yakiwa ni Ukosefu wa Pesa kwaajili ya Kujiendesha na Kwa baadhi ya hifadhi kukosa nyumba za Wafanyakazi na upungufu wa wafanyakazi kwa baadhi ya hifadhi hizo.

Mbali na Changamoto hizo pia wakuu wa hifadhi walielezea mafanikio yao katika hifadhi hizo katika vipengele tofauti tofauti kama Vitendea kazi, Ujumuikaji wa jamii katika hifadhi hizo, Utalii, Rasilimali watu, Uhifadhi Utawala na mengineyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...