UTAFITI uliofanywa na magazeti makubwa yanayoaminika nchini Afrika ya Kusini ya Mail na Guardian baada ya kushindanisha makampuni mbalimbali kutafuta orodha ya makampuni bora na yanayoaminika nchini humo yaliitaja Kampuni ya Vodacom jana kuwa ni kampuni inayoongoza kwa kuwa na mtandao bora na wa kuaminika nchini humo.
Vodacom imetangazwa kutokana na utafiti huo uliofanywa na magazeti hayo katika hafla ya kutangaza makampuni bora ilifanyika jana katika hoteli ya Sandton mjini Johannesburg.
Utafiti wa magazeti hayo kutafuta makampuni bora ulifanywa kwa ushirikiano na taasisi ya utafiti ya Plus 94 na kampuni kubwa zipatazo 167 zilishindanishwa ambapo kwa upande wa kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano Vodacom imekuwa kinara kwa kushika nafasi ya kwanza na kushika nafasi ya tatu kati ya makampuni yote yaliyoshirikishwa kwenye utafiti huo.
Ushindi huu ni mfululizo kwa kampuni ya Vodacom kwa kuwa hivi karibuni ilitangazwa kuwa mwajiri bora nchini Afrika ya Kusini.
Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom, Maya Makanjee amesema, “Siri ya mafanikio na kupata ushindi wa tuzo mbalimbali ni kufanya kazi kwa uwazi, umakini na kuwathamini wafanyakazi wake,wateja na wabia wote inaoshirikiana nao katika biashara”
Makanjee alisema Vodacom inajivunia kwa ushindi huo na unaipa moyo wa kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja na kushiriki katika kusaidia jamii inapofanyia biashara. “Tunazidi kufarijika kwa kupata tuzo mbalimbali na hii inazidi kutupa moyo wa kufanya vizuri zaidi na tutazidi kutoa huduma bora kwa wateja wetu, jamii,wabia wetu na kuwajali zaidi wafanyakazi wetu ili kukuza zaidi biashara yetu” aaliongeza Makanjee.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...