Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto kabla,wakati na baada ya uchaguzi,lakini pia viongozi wa vyama vya siasa,wagombea na wanachama kuheshimu na kutekeleza sheria,kanuni,maadili na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria nyinginezo za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa.
Fuatilia matukio katika picha hapa chini-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua kikao hicho cha wadau ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuona amani ya nchi inavurugwa hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa watu wote watakaofanya vurugu siku ya uchaguzi.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...