Mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa akiwa katika mkutano wa hadhara.
BARAZA la Wanawake la Chama Cha Demokrasia (Chadema) Taifa, Bawacha, limewataka wanawake nchi nzima kupiga kura na kukaa mita 200 ili kulinda kura zao kwani ni haki yao kisheria.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha Kunti Yusuph wakati wa mkutano na wanawake, uliofanyika katika ofisi za Chadema kanda ya ziwa Victoria jijini hapa.
Kunti ambaye ni mratibu wa mikutano ya kukutana na wanawake ya mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa, amesema kuwa kupitia wanawake wa Mwanza, wanawake nchi nzima wanapaswa kupiga kura na kulinda kura zao.
Amesema endapo wanawake na watanzania kwa ujumla watapiga kura na kuondoka watakuwa wamevunja sheria ya nchi hivyo amewaomba kulinda kura zao kwani ndio maisha yao.
Hata hivyo Regina aliwaomba wanawake na watanzania kwa ujumla kupiga kura kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais kwa maendeleo ya Taifa.
msidanganywe akina mama, mtaumizwa, hakuna mtu atakayewasaidia, sanasana mtaambiwa poleni kwa yaliyowafika, halafu watu wanajirudia nyumbani kwao kuendendelea na maisha.
ReplyDeletePIGA KURA RUDI NYUMBANI KASUBIRI MATOKEO.
PLEASE MSIDANGANYIKE MSIDANGANYIKE, FIKIRIENI WATOTO WENU.
Tatizo mnafosi mambo ya magogoni yanakuja kiupole na si kulazimisha watu kina Mama zangu na Dada zangu wata kusikilizeni lakini Jumapili wote Magufuli na Mama Samia haiingii akilini uwaambie wanawake walinde?
ReplyDeleteUjumbe kwako mama Regina, wakina mama tuna shughuli nyingi majumbani mwetu, hatutaweza kushinda mita 200 kuzilinda kura,
ReplyDeletetunatumaini kuwa wakala mliowachagua wapo imara na
wataifanya kazi kuhakikisha kura
zinahesabiwa vizuri. Labda we mwenzetu, watoto wako wamekuwa wakubwa unaweza kushinda kituoni kulinda kura zisiibiwe, utakuwa kituo gani na kuanzia saa ngapi? Naweza mtuma myu akuletee maji ya kunywa
Au ndio ileee 'lasti miniti doti komu' hata umlishe nyasi za mbuga nzima, kwa siku moja tu tena ya mnada, abadani awe Mbuzi, Ng'ombe, Punda n.k. hawezi kunenepa.
ReplyDelete#HAPA KAZI TU: "JOHN POMBE MAGUFULI na MAMA SAMIA SULUHU". Khalaaaaaaaaas!