Mwanafunzi Fuad Thabit kutoka Feza Boys Secondary aliyeibuka mshindi wa kwanza shule za sekondari katika Shindano la Genius-Cup akipokea cheti na zawadi yake ya shilingi 300,000 toka kwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia.
Wanafunzi Sita Washindi wa Shindano la Genius-Cup (mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao mara baada ya kuibuka washindi. Nyuma yao ni meza kuu katika hafla ya kuwazawadia ikipata picha ya ukumbusho na mabingwa hao. 
Baadhi ya wanafunzi walioingia fainali katika shindano la kuwatafuta washindi wa shindano la Genius-Cup wakifuatilia hafla hiyo jana.

WANAFUNZI Sita walioibuka mabingwa wa Shindano la Genius-Cup la masomo ya sayansi na hisabati wamezawadiwa zawadi zao jana katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika katika Shule ya Wavulana ya Feza Sekondari iliyopo Tegeta Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa shindano hili, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza, Ibrahim Yunus alisema wanafunzi sita walioibuka washindi na kupatia vitita vya fedha ni pamoja na Fuad Thabit mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary aliyejipatia shilingi 300,000 na Zulfa Khamis msindi wa pili toka shule za sekondari Mkoani Tanga aliyejishindia shilingi 200,000.

Bw. Yunus alimtaja mshindi mwingine wa kwanza shule za msingi ni Mvano Michael Cabangoh kutoka shule ya Green Acres aliyejishindia shilingi 300,000 na Shammah Kiunsi mwanafunzi wa shule ya msingi kutoka Mkoa wa Mbeya aliyejishindia kitita cha shilingi 200,000 pamoja na Dorice Ernest Msafiri mshindi wa tatu (msingi) kutoka Mkoa wa Dodoma Ignatius School aliyejinyakulia shilingi 150,000/-.

Akifafanua zaidi Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Wavulana ya Feza, Bw. Yunus alisema wanafunzi walioingia fainali na kukutanishwa kwa pamoja ni 70 kati ya wanafunzi 1,486 walioshiriki katika kinyang'anyiro hicho. Aliongeza kuwa hii ni mara ya pili shindano la GENIUS CUP linafanyika kwani kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka jana huku likilenga kukuza mapenzi ya masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi wa Tanzania.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fredrick Shuma akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi washindi aliupongeza uongozi wa shule za fedha nchini kwa kuliendeldeza shindano hilo kwani linachangia kuleta chachu ya mapenzi kwa masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi nchini Tanzania ambao wamekuwa wakiyaogopa masomo ya sayansi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...