Picha hii kutoka maktaba inamwonyesha mtoto ambaye anatumika kama askari na hivyo kumnyima haki yake ya msingi ya kuishi utoto wake, pamoja na kupata huduma zake za msingi kama vile afya, elimu, malenzi na ukuaji wenye hadhi. Pamoja na Umoja wa Mataifa kuendelea na kampeni yake ya kupinga watoto kutumika kama askari, bado taarifa za hivi karibu za Umoja wa Mataifa, zinaeleza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika katika baadhi ya maeneo kama askari, huku wengine wakiingizwa katika biashara haramu zikiwamo za ngono.
Bw. Suleiman Said Ali. Afisa Mambo ya Nje , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ( ZNZ) akifuatilia Majadiliano ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, iliyokuwa ikijadili kuhusu masuala ya misaada ya ulipuaji wa mabomu ya Ardhini, Bw. Ali pia alishiriki katika Majadiliano ya Umalizwaji wa Ukoloni kwa Makoloni 17 ambayo bado hayajapata fursa ya kujitawala na kujiamulia mambo yake yenyenyewe likiwamo Koloni la Western Sahara, koloni pekee barani Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...