Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT) Wililo Lukelo akitoa salam za rambirambi kwa niaba ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini wakati wa mazishi ya bondia Michael Yombayomba, yaliyofanyika Kibaha mkoa wa Pwani jana.
Promota wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Jay Msangi akishirikiana na waombolezaji wengine kubeba jeneza la marehemu Michael Yombayomba wakati wa safari ya kuelekea kwenye mazishi yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani jana.
Waombolezaji wakielekea mazikoni.


Mtoto wa marehemi Michael Yombayomba, Zakaria Yombayomba akiwasha mshumaa katika kaburi la baba yake.Picha na SUPER D BOXING NEWS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Serikali kupitia Jeshi la Polisi haimkumtendea haki shujaa huyu aliyewahi kung'arisha jina la Tanzania ulimwenguni!!!! Lawama hizi pia haziwezi kuepukwa na aliyekuwa kocha wa Taifa wa ngumi enzi zile, Nassoro Michael.
    Marehemu alifariki akiwa na donge la roho, hii ni mbaya sana.
    Kullu nafsin dhaaikatul maut, tujitahidini tusiwe wakatili.

    ReplyDelete
  2. Nimesoma makala ya Michael Yombayomba ...kwenye gazeti la mwananchi , imenisikitisha sana ...kwa kweli namna Bondia pekee kuliletea taifa medali kwenye mashindano ya olimpiki [ madola ] alivyoishia mwisho wa kusikitisha ....

    Michael Yombayomba anastahili kuenziwa zaidi ..hata kama akiwa hai hakuenziwa vya kutosha .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...