Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Jamani TB Joshua hana ratiba yoyote kuonana na watanzania kwa ajili ya maombi����
ReplyDeletekama hyo ratiba ipo tujuzwe plse.
Welcome dad...Glory to God. Can we have a chance to see him to pray for us
ReplyDeleteKama ana ratiba ya maombezi jaman mtujuze pleaae
ReplyDeleteTunaomba tupate taarifa kama atakua na maombezi jamani
ReplyDeleteHii inaonyesha ni politics fix nasidhani kama wameeleweka. Tumechoka na maigizo. King majuto anatosha. We need maendeleo not upcountry guys
ReplyDeleteMungu ni mwema saana. Sikutegemea kama itatokea mtumishi huyu wa Mungu angekanyaga ardhi ya Tanzania. Binafsi naomba apate wasaa wa kufanya maombi ya pamoja na wa Tanzania.
ReplyDeletehizi biashara za udini na siasa wapi na wapi? hawa wote ni wafanyibiashara
ReplyDeleteviongozi wetu kuwe makini na watu hawa
Tunaomba sana tupate ratiba ya maombezi na kama sio hivyo basi tunaomba arudi tena Tanzania kwa ajili ya kuombea watanzania kwani tuna kiu sana ya maombi yake. Amen. Natumaini mheshimiwa Rais John Magufuli atapatiwa hizi comments ili aweze kuona uwezekano wa kumuomba arudi tena Tanzania. Mungu ibariki Tanzania. Raisi umeanza vizuri na Mungu na utamaliza na Mungu.
ReplyDeletewell come papaa in tanzania.we real happy to c u in our land
ReplyDeleteNi vizuri wakristu wajue wana mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu kupitia mwokozi wao, hii kusikia mara watu wanasafiri kuombewa, wakati uwezo wa kuomba tunao, wakati mwingine ni kukosa kuelewa mafundisho ya Biblia na ni hatari inayoweza kukuingiza kwenye imani za kuabudu mwanadamu au kuingia dini zisizoeleweka. Ni tahadhari muhimu kwa wakristu wa Tanzania kumjua Mungu binafsi na kutofuata tu mkumbo.
ReplyDeleteThis mark the new era to our nation. The coming of the Prophet to our country is the sign of blessing.
ReplyDeleteKazi ipo imani hizi.
ReplyDeleteHuyu jamaa alitabiri kwamba lowasa angeshinda uchaguzi.
ReplyDeleteRAIS MTEULE NAKUOMBA SANA UTIMIZE AHADI ZAKO KWANZA USITUCHAGULIE MAWAZIRI WENGI TOKA AWAMU ILIYOPITA,MIMI NIMEKUPIGIA KURA NATAKA MABADILIKO SIYO YA KUTUTEULIA MAWAZIRI AMBAO NI WAPENDA RAHA,(NAKUMBUKA WAZIRI MMOJA AWAMU ILIYOPITA KILA WIKI YUPO ARUSHA),OFISINI HAKAI MTAKA MISIFA TU SAFARI ZA NJE ZISIZOISHA WATU KAMA HAWA HAWATAKUSAIDIA KWA CHOCHOTE ZAIDI YA KUKUHARIBIA KATIKA SERIKALI YAKO MPYA TUNAYOITEGEMEA ITALETA MABADILIKO KWA HALI YA SASA
ReplyDeleteWe'll come servant of God to our land
ReplyDeleteWe'll come servant of God to our land
ReplyDeleteProphet T.B. Joshua...da..no dought Dr. Magufuli ni chaguo la Mungu.
ReplyDeleteHa ha haa! ombeni wenyewe kwa Mwenyezi Mungu, muongeze na bidii ya kufanya kazi, bila ya shaka Yeye atawasikia moja kwa moja hakuna 'care of'.
ReplyDeleteSheeeeda bongo!!!
ReplyDeleteWote wagombea ni wasanii. Watanzania achaneni na siasa. This is mind game.
ReplyDeleteWote wasanii. Achaneni na siasa. This is mind game.
ReplyDeleteI am a Christian who voted for Dr Magifuli but here I have to take an exception. Why would he bring a foreign religious leader into an event quintessentially Tanzanian. What happened to the tradition of having the triumvirate etc of our national religious leaders? Dr. Magufuli, this is not a good start regardless of your best intentions. Am sorry.
ReplyDeleteTunataka mawaziri 15. Orodha au idadi ya wizara naifanya iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:
ReplyDelete1. Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
2. Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi.
3. Habari, Utamaduni na Michezo.
4. Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
5. Ulinzi na JKT.
6. Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; na Sheria (Katiba na Utawala Bora).
7. Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto.
8. Afya na Ustawi wa Jamii.
9. Mazingira, Nishati, Madini na Miundombinu.
10. Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana.
11. Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika.
12. Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko).
13. Kilimo, Ushirika, Uvuvi na Mifugo.
14. Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge; na Mambo ya Ndani na Uhamiaji.
15. Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia.
Watumishi wa serikali walioko katika Wizara hapo Dar es salaam wapelekwe mikoani, wilayani, katani na vijijini wawe karibu na wananchi ili kusukuma maendeleo kwa haraka. Sio, kwa mfano, wataalamu wa kiliomo na ufugaji kulundikana hapo Dar es Salaam.
Zaidi, sambamba na kupunguza orodha au idadi ya wizara, tufanye pia mabadiliko katika ukuaji wa mji yetu na kuongeza majiji. Kwa sasa hivi Dar imependelewa sana. Ndio maana kila mtu anahamia Dar es Salaam:
1. Dodoma: Makao Makuu ya Serikali kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa.
2. Arusha: ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.
3. Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi.
4. Kigoma: Kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, Burundi, Rwanda na na DCR Mashariki.
5. Mbeya: Kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia. Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe. Uwanja huu usaidie pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini.
6. Mtwara: Mji huu hauna budi kupewa hadhi mpya kama mji wa huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” (Tanzania, Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini). “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma la kuunganisha Tanzania na Msumbiji.