MAHAKAMA ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru leo Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.

********
Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

Hati ya Mashitaka ya Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya Mashitaka matatu  lakini Julai 22 mwaka 2015, Hakimu Mkazi Mary Moyo  alitoa  uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu  katika mashitaka mawili yaliyosalia ambalo ni kosa la pili na la tatu .

Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  ilimfungia dhamana Sheikh Ponda baada ya kukubaliana na hati ya aliyekuwa  Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), wakati huo Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam liloomba Mahakama hiyo imfungie dhamana mshitakiwa huyo chini ya Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai ya Mwaka 2002.

Hatua hiyo ya kufunguliwa kesi katika Mkoa wa Morogoro ilikuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Agosti 19 Mwaka 2013 saa Tatu asubuhi,  kumfutia kesi ya jinai  Na.144/2013 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano baada ya DPP kudai kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki katika kesi hiyo No.144/2013  kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Kusoma zaidi bofya HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ALHAMDULILLAH ALLAH AKISEMA KUN FAYAKUN HAKUNA PINGAMIZI HONGERA KWA KUVUMILIA ALLAH ATAKULIPA KWA SUBRA YAKO SHEIKH WETU HONGERA KWA KUWA IMARA ALLAH AKUTANGULIE KATIKA MAISHA YAKO MAPYA URAIANI

    ReplyDelete
  2. TAKBIIIIIIRRRRRRRR ALLAHU AKBAR

    ReplyDelete
  3. Alhamdulillah...

    Sasa kile kiwanja chetu pale temeke

    ReplyDelete
  4. joto la jiwe kaliona na katubu

    ReplyDelete
  5. Innallaha Ma3aswabirina.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...