Waziri Mkuu mpya Mh. Kassim Majaliwa.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mh. Majaliwa amepitishwa kwa kura 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote za ndio.
The mdudu, pongezi nyingi kwako hiko cheo ni kikubwa so usi mwangushe rais wetu Magufuli na na Watanzania wote tuko nyuma yenu na asiogopwe papa wa aina yoyote tunataka Tanzania mpya ya #hapakazitu na tunataka maendeleo yanayo onekana machoni mwetu.
ReplyDelete