Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatangaza Ratiba ya Uchukuaji Fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wana-CCM wote wenye sifa husika.  

Ratiba ya mchakato huo ni kama ifuatavyo;- 

i. Wana-CCM wasio Wabunge wanaoomba ridhaa ya CCM kugombea Uspika wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia Novemba 11, 2015 saa Sita Kamili mchana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam na kuzirejesha Novemba 12, 2015 kabla ya saa Kumi Kamili Jioni.

ii. Kwa wana-CCM ambao ni Wabunge wateule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoomba kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge hilo, wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia Novemba 11, 2015 saa Sita Kamili mchana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam na kuzirejesha Novemba 14, 2015 kabla saa Kumi Kamili Jioni.

Fomu hizo zitatolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib.

Imetolewa na:- 

KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
11/11/2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...