Balozi mdogo wa china hapa nchini Mhe. Zhang Biao  akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mkutano wa pili wa ushirikiano na africa utakaofanyika mwezi ujao Nchini Afrika yakusini ambao Utaongozwa na Rais wa China Xi Jinping  pamoja na wakuu wanchi wapatao hamsini katikakuangalia furusa zinazo tolewa na China katika kuleta maendeo africa
Mkutano wa pili wa taasisi ya ushirikiano kati ya China na Afrika –FOCAC- utafanyika mjini Johanesburg nchini Afrika kusini mwanzoni mwa mwezi ujao kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo. 
Balozi mdogo wa China nchini ZHANG BIAO amesema hayo wakati akizungumza na wandishi wahabari katika ubalozi wa china hapa nchini nakusema viongozi wakiwemo wakuu wa  nchi zaidi ya 50 na viongozi wa Umoja wa Afrika akiwemo Rais wa China XI JINPING wanatarajia kuhudhuria mkutano huo. 
Mkutano wa kwanza wa aina hiyo  ulifanyika nchini China na hivi sasa utafafanyika Africa kwa lengo la kukuza maendeleo na kusaidia bara la Afrika kuondokana na matatizo ya kiuchumi pamoja na afya. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...