Baada ya kuzindua kampeni inayohamasisha uwekaji akiba mwezi Oktoba, First National Bank Tanzania imemtangaza mshindi wa kwanza wa kampeni hiyo.
Kampeni hiyo inayohimiza utamaduni wa kujiweke akiba benki inawezesha mteja mmoja kati ya wanaoshiriki kujipatia zawadi nono ya shilingi milioni tano kila mwezi ambapo mshindi wa mwezi Oktoba ni Imelda Lutebinga ambaye amekabidhiwa zawadi hiyo jana na Francois Botha, Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank Tanzania.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Botha alisema wateja wanaoshinda zawadi hiyo kila mwezi bado wanaruhusiwa kushiriki tena kwa mwezi unaofuata mpaka mwisho wa kampeni hiyo.
“Inatia moyo sana kuona idadi kubwa ya wateja wetu wakishiriki kwenye kampeni hii na ni matumaini yetu kwamba itasaidia sana kuendeleza utamaduni wa kujiwekea akiba benki”.
First National Bank Tanzania ilizindua kampeni hiyo ya Weka Akiba na Ushinde mwezi Oktoba ili kuwatuza wateja wake na wateja wapya ikiwahimiza kujiwekea akiba zaidi wakati huo huo wakinufaika na kampeni hiyo.
Ikiwa ni sehemu ya kampeni hiyo inayoendeshwa kwa miezi mitatu, wateja wa zamani na wapya wanapata fursa ya kuingia moja kwa moja kwenye droo kila.
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank Tanzania, Francois Botha akimkabidhi Bi. Imelda Lutebinga hundi ya shilingi milioni tano baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya benki hiyo kuhamaisisha uwekaji akiba. Makabidhiano haya yamefanyika leo jijini Dar es salaam (Picha Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank Tanzania, Francois Botha akimkabidhi Bi. Imelda Lutebinga hundi ya shilingi milioni tano baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya benki hiyo kuhamaisisha uwekaji akiba. Makabidhiano haya yamefanyika leo jijini Dar es salaam (Picha Mpiga Picha Wetu).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...